ZAIDI YA WATU 20 WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BASI MKOANI SIMIYU.





Watu 11 wamepoteza maisha  papo hapo na mwingine mmoja kufariki  dunia akiwa njiani akipelekwa hospitali  ya rufaa ya Bugando,baada ya kutokea ajali mbaya ya gari iliyohusisha basi la abiria la kampuni ya Luhuye T 410 AWQ lililokuwa likitokea Tarime Mkoani Mara kwenda jijini Mwanza.  

 
Basi hilo liligonga nyumba kisha kupinduka leo saa tano na dakika 10 asubuhi  katika barabara ya Mwanza – Mara katika kijiji cha Yitwimila kata ya Kiloleli wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.    
Mbali na watu 12 kufariki dunia pia watu 60 wamejeruhiwa ambapo imeelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo kuwa  ni mwendo kasi wa basi hilo ambapo dereva alishindwa kumudu gari hilo likiwa katika kasi na kusababisha kugonga nyumba iliyokuwa pembezoni mwa barabara na kupinduka.
 
Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio, mkuu wa Mkoa wa Simiyu Paschal Mabiti amesema miongoni mwa abiria waliopoteza maisha katika ajali hiyo wanawake ni 5 na wanaume 7.  
 
Walioshuhudia ajali hiyo wamesema kabla ya kutokea kwa ajali  hiyo basi hilo lilianza kuyumba na kusababisha kugonga nyumba iliyokuwa kando kando ya barabara hiyo. 
 
 Mganga mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Magu mkoani Mwanza Dk Athuman Pembe alithibitisha kupokea majeruhi 60 pamoja na maiti 11.   
Amesema kati ya majeruhi hao 25  hali zao siyo nzuri wamepelekwa katika hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza, na kwamba hali za majeruhi waliobaki katika hospitali hiyo zinaendelea vizuri na tayari wengine wameanza kuruhusiwa.   
Jeshi la polisi mkoani Simiyu limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
 
Miongoni mwa abiria waliokuwemo katika basi hilo ambao wamepoteza maisha ni Pamoja na Alex Masatu (Dj Alex da Wolf) ambae alikuwa ni mfanyakazi wa Radio Metro iliyoko Mkoani Mwanza.

0 comments: