HALMASHAURI YA USHETU WAADHIMISHA SIKU YA UPANDAJI MITI LEO WILAYANI KAHAMA

0 comments
MTAALAMU YA UPANDAJI MITI KUTOKA  TUMBAKU AKITOA MAELEKEZO JINSI YA KUPANDA MITI HIYO HUKO KIJIJI CHA KANGEME KATA YA ULOWA WILAYA YA KAHAMA.

Upande wake kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu Anna Ngongi amesema uchumi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu unategemea zao la tumbaku hivyo haiwezekani kukata miti tu bila kupanda mingine ambayo itaendelea kutumika hapo baadae.
Ngongi ameeleza kuwa  zao la tumbaku linahitaji sana miti,hivyo wananchi na hasa wakulima wawe chachu ya kuhamasisha maendeleo kwa kupanda miti mingi katika maeneo yao ambapo wao ni watumiaji wakubwa.
Aidha aliwashukuru wadau walioshiriki zoezi hilo la upandaji wa miti hususani kampuni ya Tumbaku ATTT kwa kutoa elimu ya Ugani na hifadhi ya mazingira pamoja na bodi ya Tumbaku kwa kuratibu maendeleo ya zao hilo wilayani. 
Maadhimisho haya hayo ya upandaji miti katika halmashauri ya Ushetu hufanyika disemba mbili kila mwaka ambapo katika msimu wa mwaka 2014/2015 imepanga kupanda miti ipatayo 2,726,438 huku kauli mbiu ikisema “Panda Miti ikutunze”.

MTENDAJI WA KATA YA ULOWA AKIMKARIBISHA MGENI RASMI NA WAGENI KUTOKA WILAYANI KWA AJILI YA ZOEZI LA KUPANDA MITI ,ALIYEVAA TRAKISUTI  KATIKATI NI KAIMU MKURUGENZI WA HALAMASHAURI YA USHETU BI ANNA NGONGI NA WATUMISHI WENGINE WA HALMASHAURI HIYO.
PICHA ZAIDI

KAIMU MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA USHETU MH TABU KATOTO AKIONGEA KATIKA ZOEZI HILO.
BWANA TITO MWELE MKULIMA ALIYETOA SHAMBA LAKE KUPANDA MITI KAMA MKULIMA WA MFANO.


ZOEZI LA UPANDAJI LILIPAMBA MOTO LICHA YA MVUA KUBWA KUNYESHA WAKATI WATUMISHI NA WADAU WAKIENDELEA KUPANDA MITI.

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI KANGEME PIA HAWAKUWA NYUMA KATIKA KUPANDA MITI.




WADAU WAKIENDELEA KUPANDA MITI.

WADAU TOKA KAMPUNI YA TUMBAKU ATTT PIA WALIKUWEPO KATIKA KUPANDA MITI.




HABARI KUHUSU HELIKOPTA ILIYOUA WATU WANNE LEO JIJINI DAR ES SALAAM,TAZAMA PICHA HAPA

0 comments



 Sehemu ya mabaki ya Helikopta baada ya kuanguka Ajali ya Helicopter ambayo imedaiwa kuwa ni mali ya Maliasili na Utalii imegharimu maisha ya marubani 3 wa Jeshi la Polisi Tanzania. Sp Kidai Kaluse, Insp.Simba Must Simba, Pc. Josso Selestine, Na rubani mmoja Capt. Khalfan,Ajali  hiyo imetokea huko Kipunguni B Moshi Bar,Ukonga-Ilala jijini Dar es Salaam. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana mpaka sasa. 
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova 
akifafanua jambo mbele ya Vyombo vya habari katika eneo la ajali,kufuatia kutokea kwa ajali hiyo iliyopelekea vifo vya watu wanne.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaa,Mh.Sadick Meck Sadick akizungumza mbele ya Vyombo vya habari katika eneo la ajali,kufuatia kutokea kwa ajali hiyo iliyopelekea vifo vya watu wanne
 Baadhi ya Wataalamu wakifanya uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo ya Helikopta.
 Baadhi ya watu wakishuhudia mabaki ya helikopta hiyo iliyopata ajali maeneo ya Kipunguni B Moshi Bar,Ilala jijini Dar es Salaam.

HOUSE GIRL ALIYEMTESA MTOTO HUKO UGANDA AFUNGUKA MAZITO

0 comments
baby021

Baada ya story ya yule msichana kwa anayefanya kazi za ndani Uganda kuchukua headlines katika vyombo mbalimbali vya Kimataifa Duniani, leo kipo ambacho amekizungumza kwa mara ya kwanza tangu afanye kosa hilo.
Msichana huyo Jolly Tumuhiirwe ambaye kwa sasa amekamatwa na Polisi amesema sababu iliyomfanya amtese mtoto Arnella Kamanzi, ni kutokana na kuchanganyikiwa baada ya waajiri wake kutompatia pesa ili amtumie baba yake ambaye alikuwa anaumwa.
Amesema anajiona mwenye hatia kwa alichokifanya japo anadhani alifanya hivyo kama njia ya kumkanya mtoto huyo kwa kuwa alikuwa akimuona mama wa mtoto huyo akimpiga kama njia ya kumkanya.
Jolly amelalamika kuwa anajisikia vibaya pale ambapo wafungwa wenzake wamekuwa wakimtenga sana na kutaka kumpiga.



ANGALIA PICHA-MAZISHI YA BILIONEA WA BUKOBA ALIYEFARIKI AKIFANYA MAPENZI NA MCHEPUKO KWENYE GARI,MKASA MZIMA UKO HAPA

0 comments


 
Msafara wa magari ukitoka kuchukua mwili wa marehemu hospitali kuelekea nyumbani kwake.

 
Tajiri maarufu mjini Bukoba, Leonard Mtensa akichunguzwa na daktari.

KIFO cha tajiri maarufu mjini Bukoba, Leonard Mtensa (50) ambacho kimetingisha kanda nzima ya ziwa, kilichotokea dakika chache baada ya marehemu kudaiwa kufanya mapenzi ndani ya gari lake, sasa mambo hadharani juu ya kila kitu kilichotokea.

Tukio hilo lililozua gumzo mjini Bukoba, lilitokea usiku Novemba 18, mwaka huu ambapo imeelezwa kuwa marehemu ambaye ni baba wa familia, kabla ya kupatwa na umauti, alikutwa ndani ya gari yake aina ya IST lenye namba za usajili T. 982 CQG akifanya mapenzi na mchepuko wake aliyetajwa kwa jina la Jackline Hassan (25) maeneo ya Buyekere mjini Bukoba.
 
 
Mwili wa marehemu, Leonard Mtensa ukitolewa hospitali ya mkoa wa Kagera  kupelekwa nyumbani kwake kuzikwa jana.

TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio marehemu ambaye anamiliki Klabu ya Linas, alidaiwa kunywa pombe kali aina ya  Whisky Bond pasipo kula vizuri huku akisumbuliwa na tatizo la presha hivyo wakati akifanya yake ndani ya gari, ghafla presha ilipanda, akaanza kutapatapa.

“Si unajua tena jamaa umri umeenda kidogo na anasumbuliwa na presha, sasa inawezekana na kinywaji alichokunywa ndiyo kilitibua zaidi. Pombe ukiwa hujala huku una tatizo la presha madhara yake ndiyo haya,” kilisema chanzo chetu.
 
 
Mke wa marehemu akiwa haamini kama mumewe amefariki.

APEWA MSAADA
Baada ya hali yake kubadilika ghafla, inadaiwa kuwa mpenzi wake badala ya kukimbia kama ambavyo wengine hufanya, yeye alifanya juhudi kubwa kujaribu kuokoa jahazi kwa kupiga simu kwa marafiki wa marehemu, lakini kabla hawajafika, mtu mmoja alitokea na kumsaidia marehemu kumpeleka katika kituo cha Afya cha CLCT-Ndolage.

AFIA NJIANI
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, baada ya mtu huyo kujitolea kumkimbiza hospitali, hali ya Mtensa ilizidi kuwa mbaya ambapo alifariki kabla hajafika hospitali.
“Wakati wanamchukua kwenye gari, mapigo ya moyo yalikuwa yakimwenda mbio sana kabla hajafika hospitali akafariki,” kilisema chanzo chetu.
 
 
Binti aliyekuwa na marehemu.

HOFU KWA MREMBO
Chanzo kilidai kuwa, baadhi ya marafiki wa marehemu waliingiwa hofu na mrembo huyo na kuwa na wasiwasi wakihoji chinichini kwamba pengine alimpa marehemu kitu kibaya.
 
“Marafiki wa marehemu waliingiwa hofu sana na mazingira ya kifo, walikuwa wakijiuliza isije kuwa mrembo aliyekuwa naye amempa kitu chenye madhara,” kilisema chanzo chetu.
 
 
ASHIKILIWA NA POLISI
Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera, ACP Henry Mwaibambe alikiri kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema wanamshikilia Jackline kwa ajili ya upelelezi zaidi.
 
 
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu.

AIBU, SIMANZI MSIBANI
Chanzo hicho kilizidi kueleza kuwa, msibani nyumbani kwa marehemu maeneo ya Kyakairabwa, kata ya Nyanga, waombolezaji walikuwa wakiona aibu kuzungumzia kifo chake hadharani kwa kuona ni kashfa hasa kwa kuwa marehemu alikuwa mtu anayeheshimika katika jamii.
 
 
Jeneza la marehemu, Leonard Mtensa.
“Unajua hakuna mtu hata mmoja ambaye anataka kuongelea kifo cha baba huyo, hata marafiki zake hawaongei kabisa kwani wanaona kuwa ni kashfa kwa sababu Mtensa alikuwa ni mtu maarufu sana si kwa hapa Bukoba tu, bali hata jijini Mwanza na kanda ya ziwa kwa jumla,” kilisema chanzo hicho.
 
 
WHISKY BOND IPOJE?
Ili kutaka kufahamu uhusiano wa kilevi alichokutwa nacho marehemu na kifo chake, waandishi wa habari hizo walimtafuta daktari mmoja mtaalamu wa magonjwa ya binadamu, (jina linahifadhiwa) ambaye alisema kitendo cha mwanaume kupoteza maisha akiwa anafanya mapenzi ni jambo la kawaida.

“Wako watu wanaofariki wakiwa wanafanya tendo, inategemea, wengine wanakuwa na historia ya magonjwa kama shinikizo la damu, sasa ile nguvu inayotumika katika tendo na kama ugonjwa utatokeza wakati huo, uwezekano wa kupoteza maisha ni mkubwa.

“Halafu pombe kama hii ni kali, sasa kama mtu alikuwa na matatizo ya presha, akawa amezidisha kiwango ni rahisi zaidi ku-collapse (hali kubadilika) wakati wa tendo. Tatizo lingine linaweza kuwa ni aina ya vyakula anavyokula kufuatia matumizi ya pombe yenye kilevi cha juu.
 
 
Mfano wa gari aina ya IST alipokutwa marehemu.
“Maana unakuta mtu mwingine anakunywa kilevi kikali lakini hapendi kula, hili nalo ni tatizo kubwa. Vinywaji vikali mara nyingi vinaendana na ulaji wa vyakula vyenye mafuta kwa sababu hivi huenda kukausha damu,” alisema.Marehemu aliyeacha mjane na watoto, alitarajiwa kuzikwa jana mjini humo.

Chanzo Global