UGONJWA HATARI WA AINA YAKE WAIBUKA,MTU HUJIKUTA KAPIGWA MHURI WA AJABU KWENYE MWILI,UNA NAMBA,NAMBA NDO SIKU ZAKO ZA KUISHI BAADA YA HAPO UNAKUFA

Habari kutoka kata ya Mutukula wilaya ya Missenyi mkoani Kagera nchini Tanzania zinaarifu kuwa kuna ugonjwa wa ajabu ulioanzia nchini Uganda na kuua watu wengi. 

Imeelezwa kuwa mtu hujikuta ana mhuri wa namba katika mwili wake  na hufariki dunia baada ya siku za namba hiyo ya mhuri iliyopo katika mwili wake ambayo hupigwa bila kujijua.

Tayari leo 13.05.2014 katika kitongoji cha Nyakera kata ya Mutukula wilayani Missenyi mtoto mwenye umri wa miaka minne (4) amefariki dunia baada ya kupigwa mhuri wa namba 3 juzi mgongoni. 


Mwenyekiti wa kitongoji hicho na baba mzazi wa mtoto huyo wamethibitisha kutokea tukio hilo. 


Mkuu wa wilaya ya Misenyi Kanari mstaafu Issa Njiku alipoulizwa juu ya tukio hilo amesema hajapata taarifa hizo. 


Tayari kuna mtu mwingine eneo hilo ana mhuri wa namba 14 kwenye mwili wake. 

Nitaendelea kuwafahamisha kuhusiana na ugonjwa huo kadri ninavyopata taarifa.


Na Hilali Ruhundwa Malunde1 blog-Kagera

0 comments: