MSF kujaribu tiba mpya dhidi ya Ebola

Tiba mpya huenda ikaleta matumaini kwa Wagonjwa wa Ebola
Shirika la Madaktari wasio na mipaka, MSF limesema litafanya majaribio ya tiba mpya ya Ebola katika vituo vitatu Afrika Magharibi.
 
Wafanyakazi hao watatumia dawa aina mbili zilizoainishwa na Shirika la Afya duniani, WHO.
Sababu ya kufanyika kwa majaribio hayo ni kuwafanya Wagonjwa kuendelea kuwa hai wakati wa siku 14 za mwanzo tangu maambukizi ya ugonjwa huo.

Taarifa hii inakuja wakati idadi ya waliopoteza maisha kutokana na Ebola kufikia 5,160.
Ugonjwa huo umeelezwa kuathiri zaidi ya watu 14,000, karibu wote kutoka Afrika Magharibi.
Msemaji wa MSF Annick Antierens amesema hatua hiyo mpya inafanywa kwa kushirikiana na watafiti kutoka Uingereza,Ufaransa na Ubelgiji kwa lengo la kutoa nafasi ya waathirika kuwa na matumaini ya kuishi.

0 comments: