WATU ZAIDI YA 200 WANUSURIKA KUFA BAADA YA NDEGE WALIYOKUWA WAMEPANDA KULAZIMIKA KUTUA KWA DHARURA KATIKA KIWANJA KIDOGO ARUSHA ...!!


Abiria zidi ya 200 waliokuwa wamepanda ndege aina ya 5H ET-AQW mali ya Shirika la ndege la Ethiopia iliyokuwa ikitoka nchini Ethiopia Kwenda katika uwanja wa ndege wa Kimataifa mkoani Kilimanjaro (KIA) wamenusurika kufa baada ya Uwanja wa kia kuwa na hitilafu hivyo kulazimika kutua katika kiwanja Kidogo cha Kisongo jijini Arusha.
Ndege hiyo ikiwa uwanjani hapo huku tairi la mbele likiwa limezama kwenye udongo pembeni kutokana na uwanja huo kuwa mdogo
Kwa mujibu wa Taarifa zilizotufikia ndege hiyo imelazimika kutua katika uwanja mdogo wa ndege wa Kosongo ulioko Jijini Arusha, na kuzua hofu kwa watu wa eneo hilo.

Hadi sasa shughuli za uokoaji zilikuwa zikiendelea, Taarifa kuwa ni hitilafu gani iliyotokea bado hatujaipata, na pindi tutakapoipata tutakufahamisha.
Jinsi Ndege hiyo ilivyoacha uwanja na kuingia kwenye ukoka
Muonekano wa ndege hiyo mara tu baada ya kutua uwanjani hapo

Wananchi wa jiji la Arusha Wakiangalio tukio hilo  kubwa kwao
Kama inavyoonekana katika picha kikosi cha Zimamoto nacho hakikuwa nyuma
Wananchi wakiwa wamekaa kuangalia hali ilivyo
Baadhi ya watu na viongozi mbalimbali waliokuja na magari kuangalia tukio hilo
Kweli hali ilikuwa tete

Uwanja ulivyo mdogo na Ukubwa wa ndege iliyotua

Magari ya zimamoto yanazidi kuongezeka

Baadhi ya wananchi wakijaribu kufahamisha jamaa zao juu ya tukio hilo japo kwa simu
Hali ya jiji la Arusha ilivyo ya Baridi na Ukungu kwa siku ya leo

Kwa hisani ya  Emmanuel Mlelekwa - Arusha.

0 comments: