TAARIFA ZAIDI AJALI ILIYOUWA DEREVA WILAYANI KAHAMA

 
Mtu mmoja anasemekana kupoteza maisha na mwingine kujeruhiwa baada ya Magari Mawili waliyokuwa wanaendesha kugongana uso kwa uso katika eneo la Trans Oil kata ya Nyasubi Wilayani Kahama mkoani Shinyanga jana usiku.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa mbili usiku likihusisha gari aina ya Coster mali ya Kampuni ya CK Safari Tours yenye namba T-468-CAL kugongana na Semi Teller aina ya Scania yenye namba T-498-BVH.

 
Kwa mujibu wa Mashuhuda, gari aina ya Coster ilikuwa ikitokea eneo la kituo cha Mafuta kwenda Phantom, huku Scania hiyo ikitokea jijini Dar-es-salaam kwenda nchi jirani na ndipo zikagongana uso kwa uso.

Taarifa zinasema Dereva wa Scania hiyo ndiye huenda amefariki dunia huku dereva wa Coster hiyo akisemekana kujeruhiwa na kupelekwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama kwa matibabu.

Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.
 


0 comments: