Watu 17 wamejeruhiwa
baada ya gari la abiria walilokuwa wakisafiria kutoka ulowa kwenda mjini
kahama kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha Nyandekwa wilaya ya kahama
mkoani Shinyanga.
Ajali hiyo imetokea leo asubuhi ikilihusisha gari namba T 208 AGE lilokuwa likiendeshwa na dereva aliyetajwa kwa jina la
Rashid Ramadhan mkazi wa Kahama mjini, ambaye hata hivyo alitoroka baada ya
tukio hilo.
Kwa mujibu wa daktari
mfawidhi wa hospital ya wialaya ya Kahama, Deogratius Nyaga, jumla ya majeruhi
5 wamepatiwa matibabu na kuruhusiwa huku 12 wakiwa wanaendelea na matibabu
hospitalini hapo.
 |
| Mgonjwa akiwa amepumzika baada ya kupatiwa huduma |
 |
| Daktari
mfawidhi wa hospital ya wialaya ya Kahama, Deogratius Nyaga akiongea na waandishi wa habari |
Daktari Nyaga amewataja
waliolazwa kuwa ni Elizabert Mgesa (49), Katarina Makoye (32), Eliza Timotheo
(30), Ngeke Chanila (23), Zawadi Andrea (18), Amos Hussein (32) na Adam John
(20) ambaye alikuwa kondakta wa gari hilo.
Wengine ni Zakaria Leonce
(25), Mabala Paulo (28), Hamis Makala (26), John Marcel (26) na Michael Rashid
(47) na motto benad Paulo mwenye umri wa miezi mitano na kwamba wote hali zao
zinaendelea vizuri.
Jeshi la Polisi wilayani
kahama limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba uchunguzi wakubaini
chanzo chake unafanywa, huku juhudi za kumtafuta dereva wa gari hilo
zikiendelea.
HABARI KATIKA PICHA
 |
| Majeruhi akiwa na ndugu yake ambaye amekwenda kumtembelea |
 |
| Askari polisi akiwa akichukua maelezo kwa majeruhi kwenye wodi ya wanaume |
 |
| Askari wa usalama barabarani akichukua amelezo kwa majeruhi kwenye wodi ya wanawake |
 |
| Ajabu sana: Majeruhi wawili wakiwa katika kitanda kimoja |
 |
| Mama aliyejeruhiwa pia katika ajali hiyo |
 |
| Majeruhi wa ajlai hiyo wakiendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Wilaya. |
 |
| Hawa ni majeruhi walioshare kitanda kutokan ana uhaba wa vitanda,je hali ya maambukizi inadhibitiwa vipi ikiwa wote wamejeruhiwa na wanalala kitanda kimoja? | |
0 comments: