MCHUMBA WA LULU MICHAEL SI SIRI TENA.

 

 
 
 
 
 Siku chache baada ya sexy lady wa sinema za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ kutangaza sifa za

mwanaume atakayemchumbia, amejitokeza mtu anayetaka kuchukua jumla na si siri tena, Amani limenyetishiwa.

SIFA ZAKE
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa familia ya staa huyo anayekimbiza sokoni na filamu yake ya Foolish Age, mchumba huyo anaitwa Johnson lakini ni maarufu kwa jina la JR na pia ni Mkristo kama ilivyo kwa Lulu.

JR ni mfanyabiashara kigogo wa jijini Dar mwenye ‘mahela’ ya kufa mtu.
Pia mchumba huyo ni bosi wa kampuni kubwa ya uandaaji, usambazaji wa kazi za sanaa Bongo.

ALISHAKWENDA KWA AKINA LULU
“Kwa taarifa yenu, tayari JR anafahamika vizuri kwa akina Lulu kwani alishakwenda kujitambulisha na kuna maneno kwamba ndiye aliyempangia nyumba kubwa, Tegeta jijini Dar.

“Unajua yule jamaa aliona fursa akaitumia. Baada ya Lulu kutoka mahabusu kwa matatizo ya kifo cha mwandani wake, Steven Kanumba ndipo JR akafanya juu chini kumnasa hadi akafanikiwa,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:

“Muda siyo mrefu zitasikika cherekochereko za Lulu kuolewa.
“Ukweli ni kwamba hata mama Lulu (Lucresia Karugila) amemkubali yule mchumba kwani ndiye anayemfanya Lulu aonekane kama alivyo kwa sasa.

“Sasa hivi Lulu anaishi kwenye bonge la nyumba kule Tegeta (Dar) na suala la usafiri si ishu. Anabadili tu magari. Kusema kweli kwa sasa bidada mambo yamemwendea vizuri.
“Anachoogopa tu yasitokee kama yale ya Clement wa Wema Sepetu.”

AMANI LASAKA WAHUSIKA
Baada ya kumwagiwa upupu huo, gazeti hili liliwasaka wahusika mmoja baada ya mwingine ili kupata mbivu na mbichi za ishu hiyo.

MAMA LULU
Kwa kuwa ni jambo la kifamilia, gazeti hili lilipozungumza na mama Lulu, Lucresia Karugila alisema si jambo baya kwa mwanaye kuwa na mchumba hivyo anamkubali (huyo mchumba) huku akiweka wazi kuwa hana kipingamizi chochote.

Alipoulizwa jina la mwanaume huyo na kwamba ni kigogo mwenye fedha nyingi, mzazi huyo alitoa ruksa aulizwe Lulu mwenyewe.

“Mimi sina sababu ya kumkataa mwanaume ambaye wamekubaliana na mwanangu, kikubwa ni makubaliano, namkubali,” alisema mama Lulu.


HUYU HAPA LULU
Kwa upande wake Lulu mambo yalikuwa hivi;
Amani: Mambo vipi Lulu?
Lulu: Poa, naongea na nani?
Amani: (akatajiwa jina la mwandishi) kwanza hongera kwa kupata mchumba.
Lulu: Nani kawaambia?

Amani: Kwa kazi yetu hii hatushindwi kujua. Je, ni kweli umepata mchumba?
Lulu: Ndiyo lakini nisingependa sana kulizungumzia hilo.
Amani: Anaitwa nani?
Lulu: Siwezi kumtaja leo (Jumanne iliyopita). Nitawatajia tu ninyi subirini. Itakuwa surprise (mshangao), siku si nyingi nitamuanika.

Amani: Je, ni kweli ni maarufu kwa jina la JR? Au wewe tutajie hata jina la mwanzo tu.
Lulu: Nimeshasema jamani nitawatajia kwani ninyi mna haraka gani?
Amani: Je, ni kweli ni mmiliki wa kampuni ya burudani? (anatajiwa kampuni).
Lulu: Hayo yote yatafahamika kwenye utambulisho. Naomba niishie hapo ‘coz’ sina cha zaidi kuhusu ishu hiyo jamani subirini siku si nyingi.


MAMA KANUMBA
Baada ya kujiridhisha kuwa sasa Lulu ana mchumba rasmi, ‘kijumbe’ wetu alimfikishia taarifa aliyekuwa mama mkwe wa staa huyo wakati akiwa na Kanumba, mama Kanumba, Flora Mtegoa ili naye atie neno.

Mama Kanumba hakuwa na kipingamizi juu ya suala hilo zaidi ya kuchekelea huku akiweka wazi kuwa Lulu kwa sasa anaweza kuolewa.
“Mimi sina tatizo kabisa, namjua. Lulu anaweza kuolewa na nimempa baraka zote,” alisema mama Kanumba ambaye kwa sasa ni shosti mkubwa wa mama Lulu.

JR SASA
Hata hivyo, gazeti hili halikuishia hapo kwani lilisaka namba ya simu ya kiganjani ya mwanaume huyo ambapo ilipopatikana, alipigiwa, mambo yakawa hivi:
Amani: Habari yako mkuu JR?
JR: Safi, nikusaidie nini?

Amani: Mimi…(akatajiwa jina la mwandishi na kampuni) wewe ndiye JR mmiliki wa kampuni ya…(anatajiwa jina la kampuni).
JR: Kwanza mimi siyo JR ni GR. Huyo JR ni mdogo wangu.
Amani: Mbona sisi tumetajiwa JR ambaye anamiliki kampuni ya...(anatajiwa tena jina la kampuni).
JR: Oke, ndiyo mimi nikusaidie nini?

Amani: Taarifa tulizonazo ni kwamba una uhusiano na Lulu? Yaani wewe ndiye mchumba wake?
JR: Ndiyo, sitaki maswali (tusi na kukata simu).  
Tangu kitokee kifo cha Kanumba ambaye alikuwa na uhusiano wa siri na Lulu, bidada huyo hajawahi kuwa na mwanaume hadi huyo mchumba aliyejitokeza.

0 comments: