MAMA MWENYE MATATIZO YA AKILI WILAYANI KAHAMA AJIFUNGUA MTOTO SALAMA BILA MSAADA, USIKU WA KUAMKIA JANA…!!
![]() | |||
| Mama Maria Charles akiwa na mtoto wakealiyejifungua usiku wa kuamkia jana. |
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida mama mmoja mwenye matatizo ya akili katika mji wa
Kahama, mkoani Shinyanga, amejifungua salama mtoto wa kike, usiku wa kuamkia
leo bila msaada wowote, huku akiwa katika eneo la kutupia taka.
Mama
huyo Maria Charles anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 32 mwenyeji wa Mwanza, amekutwa
leo asubuhi akiwa katika eneo analoishi ambalo ni lakutupa taka zinazotoka kwa
wafanyabiashara mbalimbali mjini kahama ikiwemo mama lishe.
Baada
ya wasamaria wema kumkuta mama huyo walimsaidia kumpeleka katika hospitali ya
wilaya ya Kahama, ambapo anaendelea kupatiwa huduma za kiafya katika wodi ya
wazazi ya hopitali hiyo.
Kwa
mujibu wa Muuguzi mkuu wa Halamashauri ya Mji wa Kahama, Richard Mabagala, hali
ya kiafya ya mtoto huyo ni nzuri, na kwamba wanaangalia taratibu za kufanya ili
aweze kulelewa katika mazingira mazuri ya kumkinga kiafya.
Mganga
mfawidhi wa Hospitali ya Halmashauri ya mji wa Kahama Dk Deogratius Nyage
ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuwasaidia watu wenye matatizo
ya akili kwa kuwapeleka hospitali pindi wanapowakuta katika hali hiyo, ili kuokoa maisha ya mama na mtoto aliyezaliwa.
Hata
hivyo Dk Nyage amewataka watu wenye akili timamu kutoshiriki kingono na watu
wenye matatizo ya akili kwani kufanya hivyo ni kuongeza idadi ya watoto wa
mitaani pamoja na taifa lenye watu wenye matatizo ya akili.
Mama
huyo pamoja na wenzake wa jinsia tofauti wasiopungua kumi ni miongoni wa watu
wanaoishi katika eneo la kutupia takataka lililopo nyuma ya hospitali ya mji wa Kahama,
huku wakilala kwenye maturubai kwa kukosa nyumba za kuishi.
![]() |
| Mama huyo akichagua nguo za kubadiri kabla ya kwenda hospital. |
![]() |
| Hapa akimbeba mwanae mgongoni kwa ajili ya kwenda hospital asubuhi hiyo. |
![]() |
| Haya ndo makazi ya mama huyo na mwanae mchanga,na jengo linaloonekana mbele ndo hospitali ya Wilaya ya Kahama. |
![]() |
| Wakina mama wakiongea na mzazi na kumsihi kwenda hospitali. |





0 comments: