SERIKALI IMEAHIDI KUDHIBITI UKATILI UNAOFANYWA DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO...!!




Serikali imesema itaendelea kutekeleza  sera na mipango ya nchi ili kuhakikisha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinakomeshwa na hatimaye kujenga jamii yenye amani na furaha.

Naibu waziri wamaendeleo ya jamii, jinsia na watoto Ummy Mwalimu akihutubia katika sherehe za maadhimisho hayo.
Hayo yamesemwa leo na naibu waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia na watoto Ummy Mwalimu, katika kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika katika kata ya bugarama wilaya kahama mkoani Shinyanga.

Mwalimu amesema Tanzania bado inakabiliwa na changamoto ya ukatili wa kijnsia ambapo takwimu zinaonyeha kati ya wanawake 100 wenye umri kati ya miaka 15-49, asilimia 39 ya wanawake hao hufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia.


Aidha amesema katika takwimu zilizofanywa na wizara hiyo kwa kushirikiana na shirika la UNICEF zimeonyesha kuwa watoto watatu kati ya watoto 10 hufanyiwa vitendo vya ukatili wa kingono.

Amesema vitendo hivyo vimekuwa vikifanyika katika maeneo ambayo mtoto anajua ni maeneo salama ambayo ni majumbani, mashuleni na katika jamii ambayo imekuwa haiko tayari kutoa taarifa katika vyombo vya dola akitolea mfano dawati la jinsia, polisi na TAKUKURU.

Hata hivyo Mwalimu ameitaka jamii kutoa taarifa kwa kupiga simu ya bure katika namba 116 ili kutoa taarifa za unyanyasaji wa kijinsia na kukomesha tatizo la ukatili wa kijinsia katika jamii.
 
MATUKIO KATIKA PICHA
Naibu waziri akifungua mziki katika maadhimisho
 
 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala naye akizungunza jambo.
Wazee wa FUTUHI nao walikuwepo









Wanafunzi wa shule mablimbalia walikuwepo pia katika mahadhimisho hayo ambapo pia ni wahanga wakubwa wa vitendo vya ukatili.










0 comments: