Mume Amcharanga mapanga mkewe mwili Mzima kwa shutuma za kuisaliti Ndoa yao huko Tarime...!!
Eliza Marwa akiugulia maumivu.
MAMA mmoja mkazi wa Ronsoti, Kata ya Nyamisangura, wilayani Bomani,
Eliza Marwa,28,
hivi karibuni amenusurika kuuawa na mumewe, baada ya
majirani kufika kumuokoa kutokana na kukatwakatwa mapanga.Mama huyo aliliambia gazeti hili akiwa katika Hospitali ya Wilaya Bomani, Tarime kuwa mume wake Marwa Ogora alimkatakata mapanga baada ya kumtuhumu kuwa alikwenda kwa hawara yake badala ya kwenda kwenye mazishi ya mjomba wake huko Bunchari.
Akifafanua
zaidi, Eliza alikuwa na haya ya kusema: ‘’Mjomba alifariki na mazishi
yake yalifanyika Desemba, kumi na sita mwaka huu ambapo nilihudhuria
baada ya kumwarifu mume wangu kuwa nitahudhuria lakini alinijibu kuwa
hakuwa na fedha za kunipa ili niende kwenye mazishi.
“Nilichukua jukumu la kwenda kwa kutumia nauli yangu kwa kuwa muda
huo mume wangu alikuwa kazini na baada ya mazishi kesho yake asubuhi
Desemba kumi na saba mwaka huu nilirudi nyumbani na kumkuta mume wangu
ambaye alianza kunipiga kwa mpini wa jembe kisha panga akidai kuwa
sikuwa nimeenda kwenye mazishi badala yake nilikuwa nimeenda kwa mpenzi
wangu.
“Alinishambulia sehemu mbalimbali za mwili hususani kichwani, kidogo
anitoe ubongo, wasingekuwa majirani kuniokoa baada ya kupiga yowe
naamini angeniua kwani hivi sasa siwezi hata kuamka na masikio yameziba,
miguu ina ganzi, siwezi kutembea.
“Mume wangu Ogora amekuwa akinipiga mara kwa mara lakini kutokana na watoto tuliozaa naye nimekuwa nikivumilia mateso, naogopa kuondoka na kuacha watoto walelewa na mama wa kambo,”alidai mama huyo.
Ogora hakupatikana kuzungumzia tukio hilo kwani anasakwa na dola na afisa mmoja wa polisi wilayani hapa wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na akasema wanaendelea kumtafuta mtuhumiwa. Naye daktari wa hospitali aliyolazwa mama huyo, Nega Malico alikiri kumpokea mgonjwa huyo.
Credit: GPL


0 comments: