Na Valence
Robert- Geita
Kwatano wamekufa
kwa kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali wakdhaniwa kuiba rambirambi ya
shilingi elfu 65.
Tukio
hilo limetokea mchana
huu majira ya saa saba na nusu katika
kitongoji cha Nyantolotolo A nje kidogo ya mji wa Geita.
mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa Mzee Luhemeja alifiwa na
mjuukuu wake na baada ya kuisha msiba huo hapo jana watu wote walisambaa wakiwepo
pia watuhumiwa waliouawa.
Mashuhuda
wameongeza kuwa usiku huo watu wanaosadikiwa wanaodaiwa kuwa 8 walifika
Nyunbani kwa mzee huyo na kuingia ndani ambapo walimkuta mtoto mdogo na kumpiga
kofi baadae wakamfuata mzee wakampiga na kumuonba awapatie fedha kwa usalama
wake.
Baada ya kumpiga mzee huyo walifanikiwa kuchukua
shilingi elfu 60 zinazodaiwa kuwa ni pesa za rambirambi zilizotolewa wakati wa
msiba baada ya mzee huyo kufiwa na mjukuu wake.
Imeelezwa kuwa baada ya kuchukua pesa kwa mzee
watuhumiwa hao walimfuata mke wake ambaye jina lake halijafahamika
naye wakampiga na kumuumiza kisha kuchukua
kiasi cha shilingi elfu 5 kisha wakatokomea kusikojulikana.
Baada taarifa kusambaa kuwa kuna uvamizi
umetokea jeshi la jadi sungusungu lilianza msako na kufanikiwa kumkamata mmoja wa
watuhumiwa akiwa na damu kwenye nguo zake na kumhoji juu ya tukio hilo,
mtuhumiwa aliwataja wenzake mmoja baada ya mwingine na jeshi hilo kuwatia mbaroni wote watano.
Baada ya watuhumiwa kutiwa mbaroni wananchi wenye hasira kali walianza
kuwashushia kipigo kisha kuwachoma moto hapo hapo huku mmoja kati ya hao watano akikatwa panga kwenye
mguu na kudumbukizwa kwenye kisima na kufia humo humo.
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya wilaya Geita
Dkt Adam Sijaona amekiri kupokea miili ya marehemu majira ya saa nane na nusu
mchana wa leo na gari la polisi waliofika muda mfupi baada ya tukio wakiwa na
kamanda wa polisi wa mkoa wa Geita.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita
kamishina msaidizi mwandamizi Leonard Paul amethibitisha kutokea kwa tukio na
kuwataja majina yao kuwa ni Juma Patrick Kigara,Marwa,Chacha Kigara,na wawili
waliofahamika kwa Eze na Shija na wa tano akiwa hajafahamika jina lake.
Kamanda
Paulo amesema tayari watu watatu akiwemo kiongozi wa jeshi la jadi wanashikiliwa
na polisi kwa mahojiano zaidi huku jeshi likiendelea kufanya uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka kwa mwandishi wa habari hizi kutoka mkoani Geita
Valence Robert asilimia kubwa ya wanaumme wamekimbia miji yao
kutokana na msako mkali unaofanywa na jeshi la polisi kubaini wahusika wa tukio
hilo
CHANZO: malunde.blog
0 comments: