MAJAMBAZI YAMPIGA RISASI MHINDI USONI NA KUMPORA FEDHA

Mfanyabiashara mmoja (Jina Halikufahamika) Mwenye asili ya Asia
ameshambuliwa na majambazi (majira ya saa 12 Kasoro jioni) kwa kupigwa
risasi katika paji la uso wake na kisha majambazi hao kutoweka na mabegi
mawili yaliyojaa fedha.

Hata hivyo haikujulikana kwa haraka ni kiasi gani cha fedha ambacho
kilikuwemo katika mabegi hayo, baadhi ya mashuhuda wa tukio walidai kuwa
majambazi hao walikuwa watatu na mmoja alikuwa na bunduki aina ya SMG.

Wakielezea tukio hilo baadhi ya wafanyabiashara wengine katika maeneo
hayo ya mtaa wa Lindi na Kongo (Kariakoo) walidai kwamba Mfanyabiashara
huyo alitoka na kufunga duka lake huku akiwa na mabegi mawili na Mashine
ya kutolea Risiti ya EFD na kuelekea katika gari lake dogo aina ya
Suzuki Carry na Ghafla walitokea watu wawili waliokuwa katika pikipiki
na mmoja wa tatu alikuwa amesimama pembeni kidogo na gari hiyo na kisha
kuelekea moja kwa moja katika gari hiyo na kumpiga risasi mfanyabiashara
huyo aliyekuwa akijiandaa kuondosha gari lake.

"Niliona watu kama wanagombania begi hivi ghafla nikasikia mlio wa
risasi na kisha nikaona pikipiki mbili aina ya boxer zikija kwa kasi
kutokea upande wa mtaa wa gerezani na kisha mlio wa pili wa risasi
ulikika tena, nahisi ndio uliokuwa umemlenga yule “mhindi” na baada ya
hapo kitendo kama cha dakika mbili hivi wale jamaa wakapokezana lile
begi na kisha kupiga risasi nyingine juu basi hapo wote tukaanza kufunga
maduka yetu na wale majambazi wakatoweka kirahisiii”
Hata hivyo baadhi ya watu wamelaumu utaratibu wa wafanya biashara wengi
wa kariakoo kuhifadhi fedha nyingi katika maduka na badala yake
wamewataka wafanyabiashara hao kutafuta mbinu mbadala itakayowaezesha
kuweka fedha na mali zao salama kabisa ikiwa ni pamoja na kutumia huduma
za kuhamisha fedha kwa kutumia mitandao, cheque, na hata credit card
kuliko Cash kwani imekuwa kawaida kwa mtukio haya kujirudia eneo hili la
Kariakoo.
chanzo-patapicha
0 comments: