MTOTO AJICHOMA MOTO BAADA YA KUKATALIWA KUOA BINTI WA DINI TOFAUTI
Kijana Mansur Tanko (21) mwenye dini ya kiislam amejichoma moto hadi
kufa kwa kukataliwa na baba yake kumuoa binti wa kikristo aliyempenda.
Shuhuda wa Tukio hilo Alhaji Jibrin Bala alisema Mansur amejichoma moto
hadi kufariki baada ya baba yake Tanko Mijinyawa kukataa ombi la mtoto
la kumuoa binti wa dini tofauti (mkristo)

"Monsur alikuja na ombi la kutaka baraka kutoka kwa baba yake juu ya
suala la kufunga ndoa na binti wa kikristo anayempenda, ila baada ya
kumwambia baba yake akakataa kata kata moto wake kumchumbia binti huyo,
baada ya kuona hivyo Mansur akaenda kulia kwenye moja ya kingo za
nyumba, mara ghafla tukaona moshi mweusi kwenda kuangalia tukakuta
Mansur akiwa anateketea kwa moto"
"baba na watu wengine wakajaribu kuuzima moto huo bila mafanikio, ambapo
Mansur alikuwa ameshaungua vibaya na walipomkimbiza Hospital alikuwa
ameshafariki kwa majeraha makubwa ya moto"
Msemaji wa kituo cha Polisi Taraba, bwana Joseph Kwaji amethibitisha
kutokea kwa kifo hicho na wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio
hilo
0 comments: