TAARIFA KAMILI NA PICHA 15 ZA AJALI MBAYA YA LORI LA MIZIGO NA GARI LA ABIRIA MKOANI KILIMANJARO
TAARIFA kamili kuhusu ajali hii iliyotokea maeneo ya KIA leo hii masaa machache yaliopita mkabala na kampuni ya kusaga kokoto ya Konoike au njia panda ya kwenda uwanja wa ndege wa Kilimanjaro International Airpot, Ajali hio iliyohusisha Lori la mizigo lenye namba za usajili T417 AST na gari la abiria la kampuni ya LM SAFARI lenye namba za usajili T175 BEA lililokuwa likitokea Moshi mjini kuelekea jijini Arusha.
Chanzo cha ajali hiyo kilieleza kuwa
ni Lori lililokua likitoka Arusha kwenda moshi likiwa kwenye mwendo wa
kasi mara ghafla dereva akaona ng'ombe wakifanya mambo ya kiutu uzima
katikati ya barabara Dereva akajaribu kukwepa ndio akakutana na gari la
abiria LM SAFARI uso kwa uso yani mbele kidogo ya kituo kidogo cha
KIA.
Watu zaidi ya 67 wamejeruhiwa vibaya japo hakuna alie fia hapo ila taarifa zilizoifikia Blog hii muda
huu ni kwamba madereva na makondakta wa gari hizo wote wamefariki dunia
katika Hospitali ya Rufaa ya Tengeru mkoani Arusha.
Imeripotiwa na ripota wangu mkoa wa kilimanjaro: Afande 'Dj Tindo' wa Ust Taifa kutoka KIA.
0 comments: