BINTI WA AJABU AIBUKA, AKILIA ANATOA MAWE BADALA YA MACHOZI
Binti mmoja wa miaka 12, amewaacha madaktari wakikosa jina la
ugonjwa unaomsumbua wala tiba, kutokana na kutokwa na mawe badala ya
machozi anapolia.
Saadiya Saleh, anayeishi nchini Yemen, anatokwa na
mawe madogo magumu chini ya kope za macho yake anapolia. Kama ilivyo
kwa machozi, mawe hayo huanza kutokeza mbele ya macho, kabla ya kuanguka
chini ya mashavu yake.
Video ya binti huyo akilia huku mawe hayo yakimtoka ilionyeshwa na kusambazwa kwenye mitandao na televisheni ya Azal iliyopo nchini Yemen.
Video ya binti huyo akilia huku mawe hayo yakimtoka ilionyeshwa na kusambazwa kwenye mitandao na televisheni ya Azal iliyopo nchini Yemen.
Video hiyo inaonyesha Saadiya akiwa amelala
kitandani, akiwa amezungukwa na madaktari na jamaa zake, huku akitokwa
mawe hayo yaliyokuwa yakidondokea kwenye nguo zake, kama ishara ya
machozi. Baadaye daktari alionekana ameshika kusanduku kidogo,
kilichojaa mawe yaliyomtoka msichana huyo baada ya kulia kwa saa chache.
Kwa mujibu wa Gazeti la Daily Mirror, madaktari
wamesema kuwa hawawezi kuitolea maelezo hali ya Saadiya kwa sababu hadi
sasa hawajui ugonjwa unaomsumbua. Hata hivyo, wananchi wamesema hofu yao
ni kuwa msichana huyo ameingiliwa na majini au ni mchawi.
“Hali hii imesababisha hofu katika eneo ambalo msichana huyu anaishi,” alisikika mtangazaji alipotoa maelezo katika video hiyo.
“Wengine wanasema msichana huyu anaweza kuwa
anatumiwa kwa mambo ya uchawi, huku wengine wakisema inaweza kuwa
mashetani. Wengine wanahofia inaweza kuwa mwanzo wa janga la
hatari,”alieleza mtangazaji huyo
Imeandaliwa na Herieth Makwetta na Mtandao
Categories:
0 comments: