HATARI...!! VIBAKA WAWILI WAUWAWA NA WANANCHI WILAYANI KAHAMA...!! SAMAHANI KWA PICHA HIZI..
Miili ya marehemu hao baada ya kupakizwa katika gari la polisi wilaya ya Kahama |
Watu wawili wanaosadikiwa
kuwa ni wezi wameuwawa leo na wananchi wanaotajwa kuwa na hasira kali katika
mtaa wa Mayila kata ya Nyihogo wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Tukio hilo la mauaji
limetokea leo majira ya saa tisa alasiri baada ya vijana hao kuhisiwa kuhusika
na matukio ya wizi ambayo yamekuwa yakitokea katika eneo hilo mara kwa mara na
kuwakosesha amani wananchi.
Gari la polisi wilaya ya Kahama likiwa limezungukwa na wananchi eneo la Tukio |
Kwa mujibu wa Diwani wa Kata
ya Nyihogo Amos Sipemba, aliyefika eneo la tukio mara baada ya mauwaji hayo,
amesema hadi sasa mmoja wa marehemu ametambulika kwa jina la Joseph Bakuku huku
mwingine akiwa bado hajafahamika.
Sipemba amesema huenda
kufanyika kwa mauwaji hayo kunatokana na wananchi hao kuwahisi vijana hao
kuhusika katika matukio mawili ya uvamizi yaliyotokea usiku wa kuamkia jana katika
kata hiyo na kuripotiwa ofisini kwake.
Jeshi la Polisi wilayani
Kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba miili ya marehemu hao
imehifadhiwa katia chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Wilaya ya
Kahama, huku uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.
0 comments: