BIDII YA KAZI YAMPA TRAFIKI HUYU MILIONI 2
Kwa wale wapitao Mwai Kibaki Road zamani Old Bagamoyo Road watakuwa
wanamjua Askari huyu ambaye amekuwa akijituma vilivyo pale darajani
Mlalakuwa, Kawe... .. Jamaa alikuwa akimbii mvua, yuko mapema asubuhi,
yuko usiku na achoki...labda tu kama ana weakness zake mchana kama vile
kwenda kuganga njaa sehemu nyingine kama ilivyo desturi ya askari
wengine wa usalama barabarani..
At last, juhudi zimelipa amejishindia Million 2... Naungana na wote alioridhishwa na kazi yake katika kumpongeza...na kumwomba Mkuu angempa hata ka V kamoja zaidi.. ..
At last, juhudi zimelipa amejishindia Million 2... Naungana na wote alioridhishwa na kazi yake katika kumpongeza...na kumwomba Mkuu angempa hata ka V kamoja zaidi.. ..
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar
es salaam Suleiman Kova(watatu toka kushoto) akiwa kwenye picha ya
pamoja na Askari wa usalama barabarani ,Moses
Alphage(wapilikushoto)aliyeibu ka kidedea kwenye program ya kuhamasisha
na kupongeza utendaji kazi wa askari wa usalam barabarani jijini Dar es
salaam iliyonedeshwa na kituo hicho cha Redio na kujishindia Sh 2
Milioni. Wa kwanza kushoto ni Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Albert
Maneno na kulia ni mtangazaji wa Clouds Said Mohamed maarufu Bonge.

Mfanyakazi wa Idara ya Masoko wa Kampuni ya Vodacom Albert Maneno (wa
tatu kushoto) akiongea kabla ya kukabidhi Sh. 2 milioni kwa askari wa
kikosi cha Usalama Barabarani Moses Alphage (wa kwanza kushoto)
aliyeibuka kidedea katika program ya kuibua hamasa ya kazi kwa askari
hao jijini Dar es Salaam iliyoendeshwa na kituo cha Redio Clouds FM.
Fedha hizo zimetolewa na wafanyakazi wa Vodacom pamoja na wananchi
mbalimbali walioguswa na programu hiyo. Wa kwanza kulia ni Kamanda wa
Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova
akimkabidhi Askari wa usalama barabarani ,Moses Alphage fedha taslimu
Sh. Milioni 2 zilizochangwa na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na
wasikilizaji wa kituo cha Redio Clouds FM kupitia program ya kuhamasisha
na kupongeza utendaji kazi wa askari wa usalam barabarani jijini dar es
salaam iliyonedeshwa na kituo hicho cha Redio.

Askari wa usalama barabarani ,Moses Alphage,akiondoka zake kwa mwendo wa
kikakamavu mara baada ya kukabidhiwa cheti na pesa taslimu kiasi cha
zaidi ya shilingi milioni 2 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es
salaam Suleiman Kova.
Kwa hisani ya wavuti
Kwa hisani ya wavuti
0 comments: