WATU WAWILI AKIWEMO MWANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA WAFA MAJI MKOANI SINGIDA...!!
Mwili
wa mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Ipembe
mjini Singida Rashid Said (16) (kushoto) na wa kijana ambaye
hajafahamika jina aliyekuwa anajaribu kumwokoa mwanafunzi.Vijana hao
wawili waliofariki dunia Machi 08 mwaka huu saa nane mchana ,mwanafunzi
huyo amefariki dunia baada ya Mtumbwi waliokuwa wameupanda kupigwa na
upepo na wao kutumbukia ndani ya maji.
Mwili
wa mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya sekondari Ipembe Rashid
Said, ukiingizwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya
mkoa mjini Singida.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
MWANAFUNZI
wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Ipembe mjini
hapa,Rashid Saidi (16) amefariki dunia baada ya mtumbwi aliokuwa
umeupanda ziwani, yeye na baadhi ya wanafunzi wenzake kupigwa na upepo
mkali na kusababisha mtumbwi kupinduka na wao kutumbukia kwenye maji.
Kijana
mmoja ambaye sio mwanafunzi na jina lake bado
halijapatikana,alijitolea kumwokoa mwanafunzi huyo,lakini naye kwa
bahati mbaya alifariki dunia baada ya kunywa maji mengi na kuzama
ziwani.Tukio hilo la kusikitisha limetokea machi nane mwaka huu saa
nane mchana.
Inadaiwa
kuwa wanafunzi hao baada ya kumaliza kipindi cha’tuition’ shuleni
kwao,kama kawaida yao walienda ‘pikiniki’ katika ziwa la Kindai na
kuanza kuogelea pembeni mwa ziwa hilo.
Askari
kutoka kikosi cha zima moto mjini hapa,Bahati Hemed,amesema kwa mujibu
wa taarifa alizopewa na mashuhuda wa tukio hilo,ni kwamba baada ya
wanafunzi hao kumwagwa ndani ya maji,baadhi ya wanafunzi walifanikiwa
kujiokoa na Rashid ambaye hana uzoefu wa kuogelea,alizama nada ya maji.
Amesema
wanafunzi hao baada ya kutoka nje ya ziwa,walimwomba kijana mmoja
ambaye alikuwa na umri mkubwa aingie ziwani ili akamwokoe mwanzao.
“Yule
kijana aliyejitolea kumwokoa mwanafunzi, alipokaribia alikotumbukia
mwanafunzi huyo, na yeye mambo yalimwendea vibaya na hivyo kutupikia
ndani ya maji na kusababaisha na yeye apoteze maisha yake”alisema Bahati
kwa masikitiko.
Alisema
baada ya hapo waliweza kuita wavuvi ambao walifika na nyavu na kuwaza
kutoa miili hiyo miwili kutoka ndani ya ziwa Kindai.
0 comments: