MTOTO AFARIKI BAADA YA KUANGUKIWA NA JABALI HUKO ILEMELA JIJINI MWANZA
Mtoto
mmoja aliyefahamika kwa Jina la Malaika Jackson amefariki
dunia Muda huu ( saa kumi jioni ) baada ya kuangukiwa na Jiwe
kubwa lililoporomoka wakati baba yake akichimba kokoto katika
mlima Giza, maarufu kama mlima wa Rada uliopo maeneo ya Kiseke,
Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza
Kabla ya kufikwa na mauti hayo, Mtoto huyu alikuwa na baba yake mzazi aliyefahamika kwa jina la Jackson Ismail, mama yake mzazi na mdogo wake wakipata chakula cha mchana baada ya kuponda mawe kutwa nzima…..

Huyu ni baba wa mtoto, bwana Jackson Ismail akimwangalia mwanae kwa uchungu…
Wangali wakipata chakula hicho, baba aliwahi kumaliza na hivyo kuendelea na kazi hiyo ya kuponda mawe huku mkewe na watoto wakimalizia kupata chakula….
Wakati bwana Ismail akiendelea kuyaporomosha mawe hayo,ghafla alisikia mtikisiko mkubwa na hivyo kumtaka mkewe na watoto watoke haraka…..Mama akiwa na mtoto mchanga waliwahi kunyanyuka na kutoka,lakini kabla binti Malaika mwenye umri wa miaka mitano hajatoka, jiwe kubwa lilimuwahi na kumkandamiza na kumfanya afariki dunia papo hapo….

Eneo la Tukio



0 comments: