UKATILI..!! MWANAMKE AUAWA KWA KUCHINJWA HUKO ROMBO MKOANI KILIMANJARO

 
Matukio ya mauaji bado yanazidi kushamiri maeneo mbalimbali hapa nchini, ambapo mauaji ya kusikitisha yametokea katika kijiji cha Mashuba wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro. 

Imeripotiwa kuwa mwanamke ajulikanaye kwa jina la Grace Pius ameuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana. 

Kwa mujibu wa shuhuda wetu aliyekuwepo eneo la tukio amesema baada ya kuzagaa tarifa hizo polisi walifika eneo la tukio kwa ajili ya upelelezi ikiwemo kuwasaka watuhumiwa wa mauaji hao.

Hadi sasa haijajulikana mara moja ni nini kimesababisha mwanamke huyo kuuawa kinyama namna hiyo. 

Hizi ni baadhi ya picha zikionesha nguo alizokuwa amezivaa marehemu kabla ya mauti kumfika huku zikiwa zina matone ya damu na alama za visu. 

Habari/Picha kwa mujibu wa mdau wetu kupitia whatsapp namba yetu +255 713 836 935
 



0 comments: