SHUHUDIA UNYAMA HUU TUNAOMBA RADHI KWA PICHA UTAKAYOONA KWENYE HABARI HII
Mwanafunzi
ambaye amefahamika kwa jina moja la LEMA Alikua akisoma mwaka wa 4 kozi
ya sheria katika chuo kikuu kishiriki cha Mt.Augustino Tawi la Iringa
(Ruaha University College-RUCO).

Taarifa
za awali zilizotufikia zimeeleza kuwamnamo tarehe 24.06.2014
mwanafunzi huyo alikua ametoka kuangalia michuano ya kombe la dunia na
akiwa amelewa akawa anatafuta chakula cha jioni na ilikua majira ya saa 5
Usiku, Mwanafunzi huyo aliingia kwenye mgahawa ambao biashara ilikua
imefungwa kwa muda huo lakini ndani kulikuwapo na Binti ambaye alianza
kupiga kelele kwa kudhani alikua mwizi. Na kwakua eneo hilo mkulikuwa na
mlinzi(Mmasai) ndiye aliyeanza kumshambulia mwanafunzi huyo.
Baada ya tukio hilo wakatokea watu
(2) waliojitambulisha kuwani askari wakaamuru mwanafunzi huyo asipigwe
kwa madai ya kumfikisha kituoni.
Lakini baada ya mwendo mfupi kuelekea
kituoni wananchi wenye hasira kali walimchukua kijana huyo kinguvu na
kwenda kumchoma moto.
Mpaka sasa Kijana huyo amelazwa katika wodi ya watu mahututi (ICU) katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa.
http://frankleonard.blogspot.com

0 comments: