Unyama!! MTOTO ABAKWA NA BABA YAKE MZAZI HADI KUFA BAADA YA KUKOROFISHANA NA MKE WAKE
MTOTO mmoja wa kike amefariki dunia mkoani Kilimanjaro baada ya kubakwa na Baba yake mzazi.
Akidhibitisha
kutokea kwa tukio hilo la kinyama, Kaimu Kamanda wa polisi mkoani
Kilimanjaro, Koka Moita, alisema tukio la ubakaji lilitokea wilaya ya
Karatu, mkoani Arusha, kabla ya kufariki kwake mjini Moshi.
Alisema
wakiwa huko Mang’ola baba huyo aitwae Elisha Wazaeli, (38), alimbaka
mtoto huyo kabla ya kurudi nae nyumbani kwao Arusha na kwamba alipofika
Arusha alikorofishana na mke wake ambae ni mama wa mtoto huyo.
Aliendelea
kusema kuwa pamoja na kupewa dawa lakini homa hiyo iliendelea
kumuandama mtoto huyo na baada ya mamake kumhoji zaidi alimwambia mamake
ya kuwa babake alimbaka.
Kaimu
Kamanda Moita aliendelea kusema kuwa polisi walimchukua mtoto huyo na
kumpeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi pamoja na tiba katika
hospitali ya Mkoa ya Mawenzi hadi alipofariki dunia Juni 4, mwaka huu.
Kwa
mujibu wa Kaimu Kamanda huyo, mtuhumiwa wa tukio hilo ametoroka na
kwamba tayari jeshi la polisi mkoani humo limeanza msako wa kumtafuta
ili hatua za kisheria zichukue mkondo wake.
Aidha
Kaimu Kamanda Moita alitoa wito kwa akina mama kuhakikisha wanakuwa
karibu na watoto wao badala ya kuwaachia wafanyakazi wa nyumbani jukumu
hilo muhimu katika malezi ya watoto.
0 comments: