WANAWAKE 100 WAFANYIWA UKATILI IKIWEMO KUPIGWA NA KUBAKWA NA WENZI WAO MKOANI SINGIDA
Wastani wa takribani wanawake mia moja mkoani Singida hufanyiwa
vitendo vya ukatili na wanaume zao ikiwemo vipigo ikifuatiwa na
ubakaji, na utupati watoto wa changa kwa wazazi kwa madai ya kutelekezwa
na wenzi wao.
Hayo yamesemwa na mkuu wa polisi dawati la jinsia mkoani Singida
Asp Ireen Mbwatilo katika ripoti ya utekelezaji wa majukumu yake na
changamoto za kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia na mpango
wa ushirikiano baina ya dawati na asasi wadau wa masuala ya kijamii na
maendeleo yake kwa kupunguza watoto wa mitaani, uzazi wa mpango na
uchumi wa familia na taifa kwa ujumla.
Aidha katika ufafanuzi wa matukio umetajwa umaskini, elimu duni na
mfumo dume miongoni mwa wamaume mkoani humo kuwa vichocheo vya
kushindwa kuwajibika kwa familia zao na kuzalisha watoto wengi wa
mitaani kwa kushindwa kuwaendeleza.
Hata hivyo katika vijiji mbalimbali baadhi ya
wanaume walikiri awali kuwa vinara wa vipigo kwa wenzi wao huku
wakieleza kuelimika kupitia mradi wa ushiriki wa wanaume kwa afya ya
uzazi na ujinsia TIMEP unaotekelezwa na serikali ya Sweden kupita asasi
za kiraia na kuahidi kuwa mabalozi wa vita ya ukatiri wa kijinsia kwa
jamii yao.

0 comments: