BASI LAPINDUKA LEO SHINYANGA, WATU 52 WAJERUHIWA LILIKUWA LINATOKA MWANZA KWENDA DAR

 
Wimbi la ajali za barabarani limeendelea nchini ambapo leo abiria 63 waliokuwa wanafasafiri kutoka Mwanza kwenda Dar es salaam na basi la Supernajimunisa T.242 BRJ wamenusurika kufa baada ya basi hilo kupinduka katika kijiji cha Busanda kata ya Samuye wilaya ya Shinyanga mkoa wa Shinyanga leo majira ya saa tatu asubuhi
Majeruhi 52 walikimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya matibabu.

Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe ameiambia malunde1 blog kuwa wamepokea majeruhi 52 ambapo kati yao majeruhi waliolazwa ni 22 na miongoni mwa ambao wanne kati yao hali zao ni mbaya na tayari majeruhi 30 wamesharuhusiwa.

Katika hatua nyingine malunde1 blog imezungumza na majeruhi waliolazwa katika hospitali hiyo ambao wamesema ajali hiyo imetokea baada ya tairi la mbele la basi hilo kupasuka na gari kupinduka mtaroni

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa uchunguzi wa awali unaonesha kwamba pamoja na kupasuka kwa tairi basi hilo lilikuwa katika mwendo kasi.
 
Kamanda Kamugisha alisema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa ajali hiyo.

0 comments: