Maajabu ya Shinyanga!! KUTANA NA JIWE LINALOSIKIA SHIDA ZA WATU,UKISEMA LINATIKISIKA
![](https://scontent-b-ams.xx.fbcdn.net/hphotos-xpa1/t1.0-9/10525640_624446170986506_6831503060186290441_n.jpg)
Mkoa
wa Shinyanga mbali na kuwa na utajiri wa madini ya dhahabu na almasi
lakini kuna mambo kadha wa kadha yaliyopo pengine huyajui na ukiyasikia
unaweza usiamini.Leo Kutana na
mwandishi Faustine Kasala anayepatikana kupitia namba 0762 935183 ambaye
ametembelea wilayani Kishapu mkoani Shinyanga na kuona maajabu ya jiwe
linadaiwa kusikia shida za wananchi.
Unayemuona
pichani ni ni Chifu Makwaia wa Utemi wa Usia akiweka sadaka yake
kwenye jiwe la Mwanzuli lililopo Kishapu mkoani Shinyanga linaloaminiwa
na jamii kuwa linajibu maswali ya watu wanaofika hapo na kuuliza shida
zao. Inaelezwa kuwa mtu ukifika katika jiwe hilo la ajabu kwanza unaanza
unaliita jina lake,lina jina jiwe hili " then unasema mimi fulani(taja
jina lako) nimekuja kuuliza je! nina UKIMWI?" likitikisika ujue imekula
kwako, au katika mishe mishe zangu leo,je nitapata pesa? likitikisika
ujue kweli utapata lisipotikisika ujue hutapata kitu.
Ni
hayo tu kwa leo tutaelendelea kuwaletea maajabu mbalimbali
yanayopatikana mkoani Shinyanga endelea kutembelea Wamtomi blog.
0 comments: