MTANGAZAJI MAARUFU WA REDIO ONE ABOUBAKAR SADIK AFANYIWA UPASUAJI, KUBWA LILILOMSIBU HILI HAPA
AFYA ya mtangazaji mwenye jina kubwa Bongo, Aboubakar
Sadik ambaye anatumikia Radio One Sterio ya jijini Dar es Salaam, si
nzuri kiasi cha kulazimika kufanyiwa upasuaji haraka.
Habari kutoka chanzo chetu cha kuaminika, zinasema kuwa, Abou
alizidiwa ghafla Jumamosi ya Julai 26, mwaka huu akiwa kazini kwake na
kukimbizwa katika Hospitali ya Hindu Mandal, Posta jijini Dar es Salaam.
“Alikuwa mzima kabisa, alizidiwa ghafla na kukimbizwa Hindu Mandal ambapo alifanyiwa upasuaji,” kilisema chanzo chetu.
Risasi Mchanganyiko lilipotaka kujua aina ya upasuaji aliofanyiwa
Abou, chanzo kikafunguka: “Ndugu yangu, suala la ugonjwa ni siri ya
mgonjwa na daktari wake, labda uwasiliane naye, maana ametoka hospitali
leo asubuhi (Jumatatu), ana nafuu nzuri.”
Aboubakar Sadik akiwa Hospitali ya Hindu Mandal, Posta jijini Dar es Salaam.
Baadaye mchana chanzo hicho kilimtumia picha mbalimbali za Abou akiwa
hospitalini hapo, ikiwemo aliyokuwa chumba cha upasuaji wakati shughuli
ikiendelea.
Mwandishi wetu alipomtafuta mtangazaji huyo kupitia simu yake ya
mkononi, hakupokea hivyo akalazimika kumtumia ujumbe uliosomeka: “Pole
kaka, nimepata taarifa unaumwa. Nini zaidi? Unaendeleaje sasa?”
Muda mfupi kabla ya kuelekea mitamboni, Abou alijibu: “Shukrani kaka.
Ni kweli, nilifanyia surgery (upasuaji) Hindu Mandal, lakini
nimesharuhusiwa, nashukuru Mungu ilikwenda vizuri.”
Abou anawika na vipindi mbalimbali Radio One vikiwemo Nani Zaidi, Chombeza Time, Mtaa wa Mangoma na Flavor 120.
Chanzo:risasi mchanganyiko

0 comments: