WAFANYABIASHARA WADOGO WADOGO WAPIGWA MARUFUKU MJINI KAHAMA
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya
Wafanyabiashara
wadogowadogo waliopo kwenye masoko yasiyo rasmi katika Halmashauri ya
Mji wa Kahama mkoani Shinyanga, wametakiwa kuondoka mara moja kabla
hawajafikiwa na Oporesheni ya kuwaondoa kwa nguvu inayoendelea katika
Halmashauri hiyo.
Hauli
hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya wakati
akiongea na wafanyabiashara wa soko jipya la Mayila lililopo Kata ya
Nyihogo ambapo amedai serikali haina utaratibu wa kila mtu kuanzisha
soko anavyotaka.
Mpesya amewataka wananchi kumpa orodha ya masoko yasiyo rasmi ikiwemo
soko la kwa Mlapa lililopo kati ya Kata za Mhungula na Nyihogo, ambalo
walishaondolewa na kuanza kurudi, na kwamba watakaokamatwa watachukuliwa
hatua za kisheria.
Awali Wafanyabiashara hao walimueleza Mpesya kuwa wanashindwa kulipa
ushuru katika Halmashauri ya Mji kutokana na biashara zao kuathiriwa na
uanzishwaji wa masoko holela mitaani hali ambayo Mpesya amesema wahusika
watakumbwa na oporesheni hiyo inayoshirikisha Jeshi la Polisi.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Nyihogo Amosi Sipemba amesema
wafanyabiashara hao wamewekeza zaidi ya Shilingi Bilioni Tatu katika
soko la mayila ili serikali iweze kunufaika ni lazima masoko ya mitaani
yaondolewe.
Akizungumzia
soko la Wakulima Mpesya amesema Wafanyabiashara katika eneo hilo lazima
waondoke baada ya kukamilika kwa soko la Majengo kwakuwa eneo hilo
Serikali hainufaiki na chochote wakati ikitumia gharama kubwa kusomba
taka za soko hilo.

0 comments: