Dharau na Ubaguzi!! AFISA HABARI WA MISUNGWI AFUKUZA WAANDISHI WA HABARI KWENYE KIKAO
KAIMU
Afisa Habari wa Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza Thomas Lutego
amewafukuza Waandishi wa Habari wa Gazeti la Tanzania Daima Antony Sollo
na Valence Robert pamoja na Twallad Sallum wa Gazeti la Mwananchi
waliofika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Misungwi ambako kikao
cha Baraza la Madiwani kilikuwa kikifanyika hapo.
Waandishi
hao waliwasili katika ukumbi huo na kukuta kikao cha Baraza la Madiwani
kikiendelea na kuingia kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao ya kupasha
habari kwa jamii, ghafla Lutego aliwaita waandishi hao na kuwaeleza kuwa
hawaruhusiwi kushiriki kikao hicho kwa kuwa alikuwa amealika waandishi
wa habari vyombo vingine.
“Naomba
mtoke ninyi mmealikwa na nani?mimi nilikuwa nimealika waandishi wane tu
sasa nawaonya iwapo mtaendelea kukaa na kufanya shughuli zenu hapa
mtaona nitakachowafanya.”alisema Lutego.
Baada
ya kutokea kwa mtafaruku huo Waandishi walitoa ripoti kwa Mkuu wa
Wilaya ya Misungwi Mariam Lugayila ili aweze kuwapa mwongozo,Lugayila
alisema.....
“kikao
hiki ni kikao cha wazi sasa kwa nini awazuie? Jamani mimi msije
mkaninukuu ila ninavyofahamu mimi kikao hiki ruksa mtu yeyote kuhudhuria
na kufuatilia mambo mbalimbali.”inakuwaje sasa mtu achukue jukumu la
kufukuza wanahabari?
Hali
hii si mara ya kwanza kwa Afisa Habari huyu kufanya fitna kwa waandishi
wa Habari na inaonekana kuna kitu kinachofichwa na Afisa Habari huyo
ili watu wasijue kinachoendelea katika Halmashauri hiyo.
Imedaiwa
kuwa halmashauri ya Wilaya ya Misungwi imekuwa na matukio mengi ya
ufujaji wa fedha za umma na huenda kualika waandishi kwa ubaguzi ni moja
ya njia ya kuzuia na kuficha maovu hayo na wameomba Mkurugenzi wa
Halmashauri achukue hatua kutatua mgogoro huo kama na yeye hahusiki kwa
namna moja au nyingine katika suala la kuzuia waandishi.
Naye
Diwani wa Kata ya Usagara Costantine Kilaga alisema “huyu bwana atakuwa
na maslahi binafsi juu ya jambo hili hiki ni kikao huru na ni cha wazi
sasa kwa nini azuie waandishi?alihoji Kilaga”
Katika
kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kilichopita Lutego
alitoa taarifa za kutumia kiasi cha shilingi laki sita 600,000 tu kati
ya shilingi milioni nane 8,000,000. zinazotengwa na Halmashauri ya kwa
ajili ya masuala ya Habari kwa mwaka 2013.
Hali
hii inaonyesha jinsi anavyowanyima haki ya kupata habari wananchi wa
Wilaya ya Misungwi na pia ni ushahidi tosha kwamba kuna siri kubwa
inayofichwa na huenda siyo maamuzi yake ila kuna kitu nyuma yake.
Wakiendelea
kutafuta haki yao ya kuhudhuria kikao hicho,waandishi wa Habari hao
walimpa taarifa Mbunge wa Jimbo la Misungwi Charles Kitwanga juu ya
kunyimwa haki hiyo ambapo Kitwanga alimwita Afisa habari huyo na kumhoji
na baada ya muda Lutego alionekana kulegeza msimamo wake huo na
kuwaacha waandishi hao kuendelea na majukumu yao.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Nathan Mshana alipoulizwa iwapo
kuna uhalali juu ya kauli iliyotolewa na Kaimu Afisa Habari Thomas
Lutego kuzuia waandishi kuingia katika kikao cha Madiwani hao Mshana
alisema hana cha kuzungumza juu ya jambo hili alijibu kwa mkato “Kikao
hiki ni cha wazi na kwamba kila mtu anayo haki ya kuingia katika kikao
hicho.”alisema Mshana.
Chanzo
cha taarifa hizi kinaendelea kufuatilia kujua undani wa chanzo cha
ubaguzi kwa wanahabari unaofanywa na Afisa Habari huyo kwa kuita
waandishi kirafiki huku akiacha kuwaalika wanahabari wengine kuhudhuria
vikao mbalimbali vya Halmashauri hiyo.
By:Malunde1 Blog
0 comments: