FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA EBOLA NA CHANZO KAMILI CHA VIRUSI VYA UGONJWA HUO NA NAMNA YA KUCHUKUA TAHADHARI

Ebola ni ugonjwa hatari unaosababishwa na virusi vijulikanavyo kwa lugha ya kitaalamu “Ebola Virus”,  ugonjwa wa damu kutoganda. 

Ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa yajulikanayo kwa ujumla kama Homa za Virusi zinaazosababisha kutokwa na Damu mwilini,(Viral Haemorrhagic Fevers) .
 
Chanzo kamili cha virusi vya ugonjwa huu hakijulikani. Katika orodha ya watu 10 waliopata kirusi cha Ebola, basi wastani kati ya watano au tisa hufa.
 
Hali inayosababisha mlipuko wake pia haijulikani.Ugonjwa huu pia hauna tiba wala chanjo.Hata dawa za jadi hazijathibitika kutibu ugonjwa huu.
 
Dalili za Ebola
Dalili za ugonjwa huu ni:-
-Homa kali  inayoambatana na kutokwa damu katika matundu yote ya mwili kama pua, njia ya haja kubwa na dogo, mdomoni, masikioni, machoni n.k.
· Kutapika damu
· Kuharisha damu
· Fizi kuvuja damu
· Kutokwa na damu na kuvujia chini ya ngozi. Kwasababu ya kutokwa na damu sehemu za haja kubwa na ndogo, choo na mkojo pia vitaonekanakuwa na damu.

 
Kuenea kwa Ebola.
Ugonjwa huu unaenea kwa urahisi sana na haraka kutoka mtu mmoja hadi mtu mwingine kupita njia mbali mbali.
Njia hizi ni:-
· Kuingia mwilini au kugusana
· Mate
· Damu
· Mkojo
· Machozi
· Kamasi
-Majimaji mengine ya mwili, ikiwa ni pamoja na jasho. 
-Kugusa mtu aliyekufa kwa ugojnwa wa Ebola kushika/kugusana na wanyama jamii ya nyani. ·
-Kuchomwa na sindano au vifaa ambavyo havikutakaswa 
-Kujamiiana
-Kugusa taka ngumu au maji taka yaliyotokana na kumhudumia mgonjwa Ebola.


Tiba ya Ebola
Hakuna tiba maalumu ya homa ya Ebola. Lakini ikiwa watu  wanapata huduma bora kutoka kwa madaktari na wauguzi, wengi wao huishi.

 
Kinga ya Ebola
Ugonjwa wa Ebola unaweza kuzuilika.Ni muhimu kwa kila mmoja kuwajibika .Njia kuu za kujikinga na ugonjwa huu:-

-Kuepuka kugusa au kuingiwa na mate, damu, mkojo, jasho, kinyesi, machozi na maji maji mengine yanayotoka mwilini mwa mtu mwenye dalili za ugonjwa wa Ebola. 
-Kwa kuwa ugonjwa huu pia huambukizwa kwa njia ya kujamiiana, epuka kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja.

-Kutoa taarifa mapema kwa viongozi wa serikali na wa huduma za Afya katika ngazi zote pale anapotokea mtu mwenye dalili za Ebola .

-Kwahi katika vituo vya huduma za Afya pale mtu anapoona dalili za ugonjwa huu. 
-Wananchi wana tahadharishwa kuepuka kushughulikia maiti ya mtu aliyekufa kwa Ebola;badala yake watoe taarifa kwa uongozi wa kituo cha huduma za Afya kwa ushauri. 
-Zingatia usafi wa mwili na tabia.

0 comments: