MAIGE AELEZEA MGOGORO WA WANANCHI WAKE KUHUSU MAKAO MAKUU YA JIMBO LA MSALALA.
Hatimaye
mbunge wa jimbo la Msalala wilayani kahama Ezekieli Maige ametoa
ufafanuzi juu ya mgogoro wa wananchi wa jimbo lake wanaogombea kujengwa
eneo la Makao makuu ya halmashauri mpya ya msalala
Akiongea kwa njia ya simu kutoka Dodoma jana Maige ambaye amewahi kuwa waziri wa Maliasili na utalii amesema suala hilo ni la kiutendaji na si la kisiasa kama baadhi yao wanavyotaka kulipeleka
Katika
halmashauri ya Msalala iliyogawanywa kutoka wilaya ya Kahama Madiwani
wake wanamvutano mkubwa wa eneo la kujenga makao makuu ya halmashauri hiyo ambapo wengine wanadai yajengwe kata ya Segese na baadhi yao wanadai kujengwa kata ya Busangi
Kufuatia
hali hiyo Maige amewataka wananchi hao watambue kuwa maombi yao hakuna
mwenye asilimia mia moja ya kukubaliwa isipokuwa maombi yote ya Segese
na Busangi yapo kwa asilimia hamsini kila mmoja
Kauli hiyo ilikuja baadhi ya wananchi hao kumtuhumu kuwa amekwamisha makao hayo kujengwa Segese hali ambayo Maige amesema yeye kama Mbunge hana mamlaka ya kugawa makao makuu ya halmashauri na kuongeza kuwa kwake wananchi wote wa Segese na Busangi ni sawa
Aliwataka
wananchi hao waelewe kuwa madiwani wao ndio waliopendekeza makao hayo
kwa muhutasari ya vikao halali ukiwemo uliopendekeza kujengwa Busangi na
ule wa kubadilisha kupeleka Segese hivyo ni uamuzi wa waziri mkuu
kumaliza tatizo hilo na si mbunge kama wanavyodai

0 comments: