MGANGA WA JADI AUA MGONJWA WAKE KWA KUMTANDIKA FIMBO NA KITU KIZITO KICHWANI WAKATI AKIMTIBU NYUMBANI KWAKE
Kijana
mmoja aliyejulikana kwa jina la Vicent Kawawa(28) ameuawa kwa kupigwa
na fimbo na kitu kizito kichwani na mganga wa kienyeji aliyekuwa
anamtibu ugonjwa wa akili nyumbani kwake katika kijiji cha Buduba kata
ya Nyandekwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha alisema tukio hilo limetokea Agosti 5 mwaka huu saa 12 jioni.
Alisema
Vicent Kawawa(28) mkazi wa kijiji cha Buduba akiwa nyumbani kwa mganga
wa jadi aitwaye Mihayo Isheli akitibiwa ugonjwa wa akili aliuawa kwa
kupigwa na fimbo na kitu kizito kichwani na mganga huyo na watu
waliokuwepo eneo la tukio na kusababisha kifo chake papo hapo.
Kamanda
Kamugisha alisema chanzo cha tukio hilo ni kwamba mgonjwa alipandisha
kichaa na kuanza kumpiga mganga wa jadi na watu waliokuwa eneo hilona
ndipo katika kumtuliza mganga alianza kumpiga akisaidiwa na watu hao
ambao idadi yao haijajulikani na kusababisha kifo chake papo hapo.
Alisema
baada ya tukio hilo mganga Mihayo Isheli alikimbia na familia yake
pamoja na watu waliokuwa katika eneo hilo na kamba jeshi la polisi
linaendelea na uchunguzi sambamba na kumtafuta mganga huyo wahusika
wengine waliokuwa katika eneo la tukio.
Na Kadama Malunde-Shinyanga
0 comments: