SHAHIDI AELEZEA JINSI ALIVYOFANYISHWA MAPENZI NA MGANGA WA JADI
Shahidi
wa pili katika kesi ya kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu
inayomkabili mganga wa kienyeji, Yahaya Michael (34) ameieleza Mahakama
ya Wilaya ya Ilala jinsi alivyoingiliwa kimwili na mganga huyo kwa
madai kwamba atampatia dawa ya kupata mto
Mwanahamisi Omary (26) alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Hassan Juma kuwa alimfahamu mganga huyo baada ya kusumbuliwa na tumbo la uzazi kwa muda mrefu.
Shahidi
huyo alidai Aprili, mwaka huu, Michael alimwambia kuwa ana majini
hivyo hawezi kupata mtoto na kumpatia dawa kwa ajili ya kunywa na
kuoga.
idai
mganga huyo alikuwa akimtibu nyumbani kwake lakini baadaye alihamishia
ofisi yake katika nyumba ya kulala wageni iliyopo Kigogo Luhanga na
kudai kuwa mganga huyo alikuwa akipaka dawa katika uume wake na
kumuingilia kimwili huku akiwa hajitambui kwa madai kwamba atamsaidia
kupata mtoto.
Aliendelea
kudai kwamba baada ya kutokuwa na mawasiliano kwa muda mrefu na
mumewe, alipata taarifa kuwa mume wake alipigiwa simu na mganga huyo na
kumtaka apeleke gari lake Toyota Rav4 lenye namba za usajili T 139 BSG
maeneo ya Jangwani kwa kuwa majini ya mkewe yanataka mtoto.
Awali,
Hakimu Juma alisema wadhamini wa mshitakiwa wanatakiwa kumtafuta
mshitakiwa huyo na kumfikisha Mahakamani hapo, aliwatahadharisha
wasipofanya hivyo kwa wakati watalipa faini ya Sh milioni sita kwa kila
mmoja.
Michael
alidaiwa Aprili 29, mwaka jana, maeneo ya Jangwani Wilaya ya Ilala,
alijipatia gari aina ya Toyota Rav4 T 139 BSG lenye thamani ya Sh
milioni 12 mali ya Eliezer kwa njia ya udanganyifu. Kesi hiyo
itasikilizwa tena Septemba 18, mwaka huu.
0 comments: