 |
Hapa
ni katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa
ngozi(Albino)wasioona na wasiosikia cha Buhangija mjini Shinyanga ambapo
leo Mjasiriamali(mfanyabiashara) kutoka Kariakoo jijini Dar es
salaam,ambaye asili yake ni mkoa wa Shinyanga(Matanda) bi Mwashi Kija
Silasi amefika katika kituo hicho na kutoa msaada wa nguo zikiwemo
suruali,mashuka mashati,na miamvuli pamoja na vitu vingine kama vile
mchele,mkaa,mafuta maalum ya kujipaka kwa watoto wenye ulemavu wa
ngozi,sukari,maharage,sabuni,mafuta ya kupikia vyote vikiwa na thamani
ya zaidi ya shilingi milioni 5.
Mbali
na kutoa zawadi hizo watoto hao ambao sasa wako 270 pia wamekula
chakula cha mchana na mjasiriamali huyo aliyekuwa ameambatana na familia
yake.Pichani hapo juu ni nguo kwa ajili ya watoto hao-Picha na Kadama
Malunde-Shinyanga |
 |
| Mpango mzima ulianzia kwenye Chakula cha Pamoja_Watoto
wakinawa tayari kabisa kula chakula kilichoandaliwa na mjasiriamali
kutoka Kariakoo jijini Dar es salaam Mwashi Kija Silasi ambaye alipata
taarifa kuhusu kituo cha Buhangija kupitia mtandao huu wa Malunde1
blog,Fahari ya Shinyanga na kuguswa na hali ya maisha magumu wanayoishi
watoto hao na kuamua kusafiri kutoka Dar es salaam hadi Shinyanga,msaada
aliotoa leo ni wa kwake kwa kushirikiana na rafiki zake wa karibu-Picha
na Kadama Malunde-Shinyanga |
 |
| Aliyeshikilia
sahani ya chakula upande wa kulia ni mjasiriamali kutoka Dar es
salaam,bi Mwashi Kija Silasi akichukua chakula kwa ajili ya kuwapatia
watoto wenye ulemavu katika kituo cha Buhangija mchana wa leo kituoni
hapo-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
 |
| Zoezi la ugawaji chakula likiendelea_Wa
tatu kutoka kushoto ni bi Mwashi Kija Silasi akishirikiana na mwalimu
mlezi wa watoto wenye ulemavu kituo cha Buhangija mjini Shinyanga bi
Maisara Adinan kugawa chakula kwa watoto leo mchana,wa kwanza kushoto ni
mmoja wa wanafamilia ya bi Mwashi walioambatana naye katika kituo hicho
akisaidia kugawa chakula-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
 |
Watoto
wanakula chakula kwa uangalizi wa karibu kabisa kutoka kwa walimu
walezi wa watoto hao ambapo hivi sasa wenye ulemavu wa ngozi wako
178,wasioona 40 na wasiosikia 52-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
 |
Chakula kilikuwepo cha kutosha,nyama kwa sana,wali kama kawaida,pilau ya kutosha,watu wote walikula na kusaza-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
 |
| Baada ya chakula_Mwalimu
mkuu wa shule ya msingi Buhangija ambaye pia ni mlezi mkuu wa kituo cha
Buhangija Jumuishi bwana Peter Ajali akimkaribisha bi Mwashi
aliyepeleka msaada leo wa chakula na mavazi katika kituo hicho ambapo
pamoja na mambo mengine alimpongeza mjasiriamali huyo kwa kuwa na moyo
wa upendo kwa watoto hao na kuitaka jamii kuiga mfano wake kwani
ameshangaa kuona akisafiri kutoka Dar es salaam kwa ajili ya watoto wa
Shinyanga-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
 |
| Katikati
ni mjasiriamali/mfanyabiashara wa nguo kutoka Kariakoo jijini Dar es
salaam bi Mwashi Kija Silasi akizungumza katika kituo hicho ambapo
alisema aliguswa na maisha wanayoishi watoto hao hivyo kuamua kuandaa
chakula cha pamoja na zawadi zingine kwa watoto hao zaidi ya 200.Alitaja
vitu alivyoleta kuwa ni nguo yakiwemo mashuka,mashati na
suruali,miamvuli,mafuta ya kujipaka na kupikia,mchele,sukari,dagaa kwa
wenye mahitaji maalum,mkaa,maharage vyote vikiwa na thamani ya mamilioni
ya fedha yote hiyo ni kwa sababu ya upendo kwa watoto hao.Nyuma yake ni
marobota ya nguo alizokuja nazo-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
 |
| Mjasiriamali/mfanyabiashara
wa nguo kutoka Kariakoo jijini Dar es salaam mwenyeji wa Shinyanga bi
Mwashi Kija Silasi akizungumza na watoto hao ambapo aliwataka,kusoma kwa
bidii kupendana,wasigombane na kujimbua na kujiamini kuwa wanaweza
kufanya mambo makubwa katika nchi hii kwani hawana utofauti na watu
wengine isipokuwa ngozi tu-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
Wa pili kutoka kushoto ni Mjasiriamali/mfanyabiashara wa nguo kutoka Kariakoo jijini Dar es salaam bi Mwashi Kija Silasi akikabidhi
Mwamvuli kwa mtoto Kabula Nkarango kutoka Kahama ambaye mwaka 2010
alikatwa mkono wake wa kulia na watu wasiojulikana na kutokomea nao
kusikojulikana.Jumla ya miamvuli 150 imekabidhiwa kwa watoto wenye
ulemavu hususani wale wakubwa kwa ajili ya kuwakinga dhidi ya jua
wanapotembea-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
 |
| Watoto wakifurahia miamvuli yao baada ya kukabidhiwa leo mchana-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
 |
| Kila
mtoto alipata shuka yake,pichani watoto wakiangalia shuka walizopewa
leo na mjasiriamali kutoka Dar es salaam ambaye alipata taarifa kuhusu
kuwepo kwa kituo cha Buhangija kupitia mtandao huu wa Malunde1
blog-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
 |
| Kulia
ni Mlezi mkuu wa kituo cha Buhangija Jumuishi Peter Ajali akiwa
ameshikilia nguo kwa ajili ya watoto wa kiume mashati na suruali
zilizoletwa na Mwanamama Mwashi kutoka Dar es salaam(kushoto
kwake)-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
 |
| Mjasiriamali/mfanyabiashara
wa nguo kutoka Kariakoo jijini Dar es salaam bi Mwashi Kija
Silasi akikabidhi sabuni za kufulia kwa watoto hao leo mchana-Picha na
Kadama Malunde-Shinyanga |
 |
| Mtoto
Kabula Nkarango ambaye alikatwa mkono wake na watu wabaya huko
Kahama.Hapa ameshikilia mafuta,sabuni,mwavuli na soda yake vyote vikiwa
vimeletwa na mwanamama Mwashi,mwenyeji wa Shinyanga lakini kikazi maeneo
ya Kariakoo jijini Dar es salaam-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
 |
| Picha ya pamoja_Mfanyabiashara
Mwashi Kija Silasi,akiwa na familia yake na watoto wenye ulemavu katika
kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu leo kituoni hapo-Picha na Kadama
Malunde-Shinyanga |
 |
| Mwalimu Peter Ajali akitoa neno la shukrani baada ya zoezi la kukabidhi msaada kuisha-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
 |
| Watoto wakibembea baada ya kula,kupokea zawadi kutoka kwa mfanyabiashara Mwashi Kija Silasi-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
0 comments: