UMESHAWAHI KUKUTANA NA MTU MFUPI KULIKO WOTE DUNIANIHUYU HAPA.
UMEWAHI KUMUONA MTU MFUPI KULIKO WOTE DUNIANI,HUYU HAPA.
Unaweza
kuwa mfupi kiasi cha kukufanya utamani kuongezeka, lakini ukiwaona
wenzako wanavyopeta nalo basi utagundua unapaswa kumshukuru Mungu kwa
umbo lolote ulilopewa.
Jyoti
Amge, mwenye umri wa miaka 21, ndiye mwanamke mwenye kimo kifupi zaidi
duniani akiwa na urefu wa inches 24 (sawa na urefu wa rula mbili za
sentimita 32).
Jyoti
ambaye ni mkazi wa Napur, India, aliingia rasmi katika kitabu cha
Guinness mwaka 2011 kama mwanamke mfupi zaidi duniani aliye hai na
tayari ameshapata deals kubwa kwa kimo chake.
Amewahi
kushiriki katika makala maalum ya Body Shock: Two Foot High Teen na
August 13, na mwaka huu alipata deal ya kuigiza katika ‘American Horror
Story: Freak Show’.
Mwanamke
huyo ambaye kimo chake kinatajwa kuwa kimetokana na tatizo la kutokua
kawaida ‘achondroplasia’ anaendelea kupiga deals kubwa na amegeuka kuwa
lulu kwa muonekano huo wa kipekee.

0 comments: