MADREVA WANAOEGESHA MAGARI VIWANJA VYA CDT. WAWATUHUMU ASKARI WA DORIA KAHAMA KUOMBA RUSHWA KWAO


 .
PICHA HII HAISADIFU UHALISIA (KUTOKA MAKTABA)

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linafuatilia uchungunzi wa askali polisi wa doria wilayani Kahama ambao wanatuhumiwa kuwanyanyasa wamiliki wa magari ya mizigo ambao huegesha kwenye eneo la halmashauri ya mji la CDT
Kauli hiyo imetolewa leo na kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga  Jastus Kamugisha wakati akiongea na RFA baada ya kutakiwa kuzungumzia malalamiko hayo yaliyotolewa kwa wandishi wa habari na wamiliki wa magari hayo
Katika malalamiko hayo wamiliki hao wamedai askali wa doria badala ya kwenda kusaka waharifu wamekuwa wakiishia kwenye maegesho ya CDT ambapo hutumia vitisho mbalimbali kwa kuwakamata madreva wanaoshindwa kuwapa rushwa kati ya shilingi laki moja hadi laki tatu  
Hata hivyo mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kahama Machibya Shidulamabambasi inayomiliki eneo hilo  la maegesho ya CDT amesema tuhuma za madai hayo atazifikisha kwa mkuu wa wilaya ya Kahama kwa kuwa ndiyo mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya
Kufuatia hali hiyo kamanda Kamugisha amesema jeshi lake litahakikisha linafuatilia tuhuma hizo na watakao bainika watachukuliwa hatua za kinidhamu kwa kufuata taratibu za kipolisi kwa kuwa kazi ya polisi ni kulinda raia wema na mali zao.
 
Credit:Shija Felician.

0 comments: