SITTI ABBAS MTEMVU NDO MISS TANZANIA MWAKA 2O14,
Mrembo
wa Redd's Miss Tanzania 2014,Sitti Abbas Mtemvu akiwa katika picha ya
pamoja na Mshindi wa pili,Lillian Kamazima (kulia) na Mshindi wa
Tatu,Jihhan Dimachk mara baada ya kutangazwa rasmi usiku wa kuamkia leo
kwenye ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam. 
Sitti
Mtemvu alianza kwa kunyakua Redds Miss Chang'ombe na baadaye Redds Miss
Temeke. Sitti ni binti wa Mbunge wa Temeke, Mhe. Abbas Mtemvu.
Kwa
ushindi huo, Sitti atapeperusha bendera ya Tanzania katika mashindano
ya Miss World 2015 na kajinyakulia kitita cha milioni 18 . 
Pichani
ni Washiriki waliochaguliwa kuingia kwenye hatua ya tano bora katika
shindano la Redds Miss Tanzania 2014 lililofanyika usiku wa kuamkia leo
ndani ya ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar.
Mmoja wa Washiriki waliongia katika nafasi ya tano bora shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakijibu maswali mbalimbali
Mmoja
wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya pichani kulia Ommy Dimpoz
akitumbuiza jukwaani akiwa sambamba na msanii Vanessa Mdee mbele ya
wageni waalikwa (hawapo pichani),waliofika kushuhudia shindano hilo.
Washiriki wa Redds Miss Tanzania 2014 wapatao 15 mara baada ya kuchujwa.
Sehemu
ya baadhi ya Wageni waalikwa wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye
shindano hilo la kumsaka Kinara wa Redds Miss Tanzania 2014 
Baadhi ya Washiriki wa shindano la Redds Miss Tanzania 2014,wakiwa jukwaani na mavazi ya ufukweni.
Msaniii
wa Muziki wa kizazi kipya Vanessa Mdee a.k.a V-Money akitumbuiza kwenye
shindano la kumsaka mshindi wa Redds Miss Tanzania 2014,yanayofanyika
usiku wa kuamkia leo ndani ya moja ya ukumbi wa Mlimani,jijini Dar.
Washiriki wa shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakikatiza jukwaani na mavazi yao ya ubunifu
Baadhi ya Majaji wakifuatilia kwa makini
Pichani ni Washiriki wa Redds Miss Tanzania 2014 wapatao 30 wakiwa jukwaani tayari kwa kuanza kuchujwa kupata washiriki 15 bora.
0 comments: