HALMASHAURI YA USHETU WAADHIMISHA SIKU YA UPANDAJI MITI LEO WILAYANI KAHAMA
MTAALAMU YA UPANDAJI MITI KUTOKA TUMBAKU AKITOA MAELEKEZO JINSI YA KUPANDA MITI HIYO HUKO KIJIJI CHA KANGEME KATA YA ULOWA WILAYA YA KAHAMA. |
Upande wake kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu
Anna Ngongi amesema uchumi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu unategemea zao la
tumbaku hivyo haiwezekani kukata miti tu bila kupanda mingine ambayo itaendelea
kutumika hapo baadae.
Ngongi ameeleza kuwa
zao la tumbaku linahitaji sana miti,hivyo wananchi na hasa wakulima wawe
chachu ya kuhamasisha maendeleo kwa kupanda miti mingi katika maeneo yao ambapo
wao ni watumiaji wakubwa.
Aidha aliwashukuru wadau walioshiriki zoezi hilo la
upandaji wa miti hususani kampuni ya Tumbaku ATTT kwa kutoa elimu ya Ugani na
hifadhi ya mazingira pamoja na bodi ya Tumbaku kwa kuratibu maendeleo ya zao
hilo wilayani.
Maadhimisho haya hayo ya upandaji miti katika halmashauri
ya Ushetu hufanyika disemba mbili kila mwaka ambapo katika msimu wa mwaka
2014/2015 imepanga kupanda miti ipatayo 2,726,438 huku kauli mbiu ikisema “Panda Miti ikutunze”.
PICHA ZAIDI
KAIMU MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA USHETU MH TABU KATOTO AKIONGEA KATIKA ZOEZI HILO. |
BWANA TITO MWELE MKULIMA ALIYETOA SHAMBA LAKE KUPANDA MITI KAMA MKULIMA WA MFANO. |
ZOEZI LA UPANDAJI LILIPAMBA MOTO LICHA YA MVUA KUBWA KUNYESHA WAKATI WATUMISHI NA WADAU WAKIENDELEA KUPANDA MITI. |
WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI KANGEME PIA HAWAKUWA NYUMA KATIKA KUPANDA MITI. |
WADAU WAKIENDELEA KUPANDA MITI.
WADAU TOKA KAMPUNI YA TUMBAKU ATTT PIA WALIKUWEPO KATIKA KUPANDA MITI. |
0 comments: