Showing posts with label MATUKIO. Show all posts

ANGALIA PICHA-MAZISHI YA BILIONEA WA BUKOBA ALIYEFARIKI AKIFANYA MAPENZI NA MCHEPUKO KWENYE GARI,MKASA MZIMA UKO HAPA

0 comments


 
Msafara wa magari ukitoka kuchukua mwili wa marehemu hospitali kuelekea nyumbani kwake.

 
Tajiri maarufu mjini Bukoba, Leonard Mtensa akichunguzwa na daktari.

KIFO cha tajiri maarufu mjini Bukoba, Leonard Mtensa (50) ambacho kimetingisha kanda nzima ya ziwa, kilichotokea dakika chache baada ya marehemu kudaiwa kufanya mapenzi ndani ya gari lake, sasa mambo hadharani juu ya kila kitu kilichotokea.

Tukio hilo lililozua gumzo mjini Bukoba, lilitokea usiku Novemba 18, mwaka huu ambapo imeelezwa kuwa marehemu ambaye ni baba wa familia, kabla ya kupatwa na umauti, alikutwa ndani ya gari yake aina ya IST lenye namba za usajili T. 982 CQG akifanya mapenzi na mchepuko wake aliyetajwa kwa jina la Jackline Hassan (25) maeneo ya Buyekere mjini Bukoba.
 
 
Mwili wa marehemu, Leonard Mtensa ukitolewa hospitali ya mkoa wa Kagera  kupelekwa nyumbani kwake kuzikwa jana.

TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio marehemu ambaye anamiliki Klabu ya Linas, alidaiwa kunywa pombe kali aina ya  Whisky Bond pasipo kula vizuri huku akisumbuliwa na tatizo la presha hivyo wakati akifanya yake ndani ya gari, ghafla presha ilipanda, akaanza kutapatapa.

“Si unajua tena jamaa umri umeenda kidogo na anasumbuliwa na presha, sasa inawezekana na kinywaji alichokunywa ndiyo kilitibua zaidi. Pombe ukiwa hujala huku una tatizo la presha madhara yake ndiyo haya,” kilisema chanzo chetu.
 
 
Mke wa marehemu akiwa haamini kama mumewe amefariki.

APEWA MSAADA
Baada ya hali yake kubadilika ghafla, inadaiwa kuwa mpenzi wake badala ya kukimbia kama ambavyo wengine hufanya, yeye alifanya juhudi kubwa kujaribu kuokoa jahazi kwa kupiga simu kwa marafiki wa marehemu, lakini kabla hawajafika, mtu mmoja alitokea na kumsaidia marehemu kumpeleka katika kituo cha Afya cha CLCT-Ndolage.

AFIA NJIANI
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, baada ya mtu huyo kujitolea kumkimbiza hospitali, hali ya Mtensa ilizidi kuwa mbaya ambapo alifariki kabla hajafika hospitali.
“Wakati wanamchukua kwenye gari, mapigo ya moyo yalikuwa yakimwenda mbio sana kabla hajafika hospitali akafariki,” kilisema chanzo chetu.
 
 
Binti aliyekuwa na marehemu.

HOFU KWA MREMBO
Chanzo kilidai kuwa, baadhi ya marafiki wa marehemu waliingiwa hofu na mrembo huyo na kuwa na wasiwasi wakihoji chinichini kwamba pengine alimpa marehemu kitu kibaya.
 
“Marafiki wa marehemu waliingiwa hofu sana na mazingira ya kifo, walikuwa wakijiuliza isije kuwa mrembo aliyekuwa naye amempa kitu chenye madhara,” kilisema chanzo chetu.
 
 
ASHIKILIWA NA POLISI
Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera, ACP Henry Mwaibambe alikiri kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema wanamshikilia Jackline kwa ajili ya upelelezi zaidi.
 
 
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu.

AIBU, SIMANZI MSIBANI
Chanzo hicho kilizidi kueleza kuwa, msibani nyumbani kwa marehemu maeneo ya Kyakairabwa, kata ya Nyanga, waombolezaji walikuwa wakiona aibu kuzungumzia kifo chake hadharani kwa kuona ni kashfa hasa kwa kuwa marehemu alikuwa mtu anayeheshimika katika jamii.
 
 
Jeneza la marehemu, Leonard Mtensa.
“Unajua hakuna mtu hata mmoja ambaye anataka kuongelea kifo cha baba huyo, hata marafiki zake hawaongei kabisa kwani wanaona kuwa ni kashfa kwa sababu Mtensa alikuwa ni mtu maarufu sana si kwa hapa Bukoba tu, bali hata jijini Mwanza na kanda ya ziwa kwa jumla,” kilisema chanzo hicho.
 
 
WHISKY BOND IPOJE?
Ili kutaka kufahamu uhusiano wa kilevi alichokutwa nacho marehemu na kifo chake, waandishi wa habari hizo walimtafuta daktari mmoja mtaalamu wa magonjwa ya binadamu, (jina linahifadhiwa) ambaye alisema kitendo cha mwanaume kupoteza maisha akiwa anafanya mapenzi ni jambo la kawaida.

“Wako watu wanaofariki wakiwa wanafanya tendo, inategemea, wengine wanakuwa na historia ya magonjwa kama shinikizo la damu, sasa ile nguvu inayotumika katika tendo na kama ugonjwa utatokeza wakati huo, uwezekano wa kupoteza maisha ni mkubwa.

“Halafu pombe kama hii ni kali, sasa kama mtu alikuwa na matatizo ya presha, akawa amezidisha kiwango ni rahisi zaidi ku-collapse (hali kubadilika) wakati wa tendo. Tatizo lingine linaweza kuwa ni aina ya vyakula anavyokula kufuatia matumizi ya pombe yenye kilevi cha juu.
 
 
Mfano wa gari aina ya IST alipokutwa marehemu.
“Maana unakuta mtu mwingine anakunywa kilevi kikali lakini hapendi kula, hili nalo ni tatizo kubwa. Vinywaji vikali mara nyingi vinaendana na ulaji wa vyakula vyenye mafuta kwa sababu hivi huenda kukausha damu,” alisema.Marehemu aliyeacha mjane na watoto, alitarajiwa kuzikwa jana mjini humo.

Chanzo Global

MAMA AJIFUNGUA MTOTO WA AJABU HUKO DAR.

0 comments
Na Dustan Shekidele, Morogoro
My God! Mama aliyetambulika kwa jina la Swaumu Sadick (25), mkazi wa Manzese jijini Dar, amejikuta yeye na manesi wakitimua mbio kwa woga baada ya kujifungua kiumbe wa ajabu.
 
Swaumu Sadick akiwa hospitali baada ya kujifungua mtoto huyo.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo ambalo kwa sasa ni gumzo, lilijiri hivi karibuni mishale ya saa 8:00 usiku kwenye Kituo cha Afya Cha Kijiji cha Mlali kilichopo wilayani Mvomero mkoani hapa.
Katika tukio hilo, ilielezwa kwamba Swaumu alijifungua kiumbe huyo wa ajabu anayedaiwa kuwa na mkia mrefu huku akiwa hana miguu.
Ilidaiwa kwamba baada ya kutokea kwa tukio hilo, baadhi ya ndugu walishikwa na taharuki kubwa huku wengine wakitoa taarifa kwa mwanahabari wetu ambaye alifunga safari kutoka mjini Morogoro na kuwasili kwenye kituo hicho cha afya majira ya saa 12:00 asubuhi.
Katika mahojiano maalum na gazeti hili juu ya tukio hilo, nesi wa zamu aliyekutwa kituoni hapo aliyejitambulisha kwa jina moja la Consolatha alikuwa na haya ya kusema: “Nilimpokea Swaumu majira ya saa 1:00 usiku akilalamika kuwa na uchungu wa kujifungua.
 
Swaumu Sadick akiuguzwa hospitali.
“Nilimpa kitanda. Saa 8:00 usiku,  uchungu ulizidi nikampeleka leba ambako alijifungua kiumbe huyo mwenye jinsi ya kiume. “Baada ya kujifungua na kumuona kiumbe huyu wa ajabu, nilitimua mbio usiku huo kwa woga na kwenda kuamsha manesi wenzangu wanoishi kota za kituo hiki cha afya.
“Nimefanya kazi hii ya ukunga na kuzalisha wazazi zaidi ya 50 lakini sijawahi kukutana na tukio kama hili.”
Kwa upande wake mganga mkuu wa kituo hicho aliyejitambulisha kwa jina moja la Dk. Beatrice alikuwa na haya ya kusema juu ya tukio hilo la kusikitisha:
“Kimsingi si kiumbe ila ni mtoto ambaye awali tulipomcheki mzazi tulibaini ana kichwa kikubwa na alishafia tumboni zaidi ya siku tatu.
“Amezaliwa akiwa na miezi nane tumboni. Tulichokifanya ni kuokoa maisha ya mama jambo ambalo tumefanikiwa.”
 
Mtoto wa ajabu aliyezaliwa na Swaumu.
Akizungumza kwa tabu na mwanahabari wetu, Swaumu alisema: “Hii ni mimba yangu ya tatu, ya kwanza iliharibika tumboni, ya pili nilifanikiwa kuzaa salama mwanangu Maimuna.
“Hii ya tatu ndiyo nimejifungua kitu hiki cha ajabu.”
Alipoulizwa kwa nini aliondoka Dar ambako ndiko kwenye hospitali kubwa na kwenda kujifungulia kijiji akijua ana matatizo ya uzazi, mama huyo alisema:
“Siku za kujifungua zilipokaribia mume wangu Abdallah aliniambia nije kujifungulia kwa bibi yangu Halima, kwa bahati mbaya ndiyo yametokea haya.”
Kwa upande wake shangazi wa Swaumu aliyekutwa akimhudumia alisema: “Yameshatokea ya kutokea, tunamshukuru Mungu na tunajiandaa kumchukua mjukuu wetu tukamzike.”

MOTO WATOKEA KATIKA JENGO LA MACHINGA COMPLEX LILILOPO ILALA, DAR ES SAALAM LEO.

0 comments
IMG-20141114-WA0005



UKATIRI UNAOTISHA HUU MUME AKATA NYETI ZA MKE WAKE NA KUZIPELEKA KWA MGANGA WA JADI ILI,APATE PESA

0 comments


Mwanamke mwenye umri wa miaka 60 aliyekatwa sehemu zake za siri (nyeti) na mumewe anayefahamika kwa jina moja la Mashaka.

Unyama wa kutisha kisa utajiri! Mwanamke mwenye umri wa miaka 60 (pichani jina linahifadhiwa), anadai kukatwa sehemu zake za siri (nyeti) na mumewe aliyemtaja kwa jina moja la Mashaka ili akauze Sh. milioni tano za Kitanzania akauze kwa mganga wa kienyeji ili apate mtaji.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo baya, mama huyo amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, Kitete ambapo anadaiwa kukutwa na kisanga hicho hivi karibuni.

Mwanamke huyo anadai kujeruhiwa na mumewe usiku wakati wakiwa wamelala nyumbani kwao Mtaa wa Kazaroho Kata ya Mbugani, Manispaa ya Tabora.

Akizungumza na mwanahabari wetu kwa tabu akiwa wodini kwenye hospitali hiyo akiwa na maumivu makali, mama huyo alikuwa na haya ya kusema:

“Siku ya tukio, nakumbuka mume wangu alikwenda kutembea, aliporejea nyumbani alifuatana na mtu mmoja ambaye ni mganga wa kienyeji.

“Walipofika nyumbani aliniambia yupo na mganga wa kienyeji ambaye alikuwa akitafuta viungo vya sehemu za siri za mwanamke akiwa na fedha milioni tano.

“Mimi nilikataa baada ya kunishawishi lakini usiku nilipokuwa nimelala, mume wangu alinikata huku akiniamuru nisipige kelele kwa kuwa alikuwa ameshapatana bei na kwamba ulikuwa ni utajiri mkubwa.”

Alisema baada ya tukio hilo alijikuta amelazwa hospitalini hapo hivyo hajui kama mumewe huyo alishakamatwa au la.

Kwa mujibu wa majirani zao, Mtaa wa Kazaroho, lilikuwa ni tukio la kutisha kwani wasamaria wema ndiyo waliomkimbiza mama huyo hospitalini ili kuokoa uhai wake.

Majirani hao walimtaka Waziri wa Maendeleo ya Wanawake Jinsia na Watoto, Sophia Simba kufanya kazi ya ziada ili sheria ichukue mkondo wake ili kupunguza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinavyoshamiri kwa kasi nchini.
Kwa mujibu wa mmoja wa madaktari hospitalini hapo ambaye hakutaka kutajwa jina kwa kuwa si msemaji, mama huyo alifikishwa hospitalini hapo akiwa katika hali mbaya lakini baadaye alipata nafuu hivyo anaendelea vizuri na matibabu.

Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Suzane Kaganda aliyehamishiwa mkoani hapa hivi karibuni hazikuzaa matunda hivyo zinaendelea.

via>>Jamvi la Habari.com

ACHOMWA MOTO AKIJARIBU KUIBIA ABIRIA WALIOPATA AJALI YA BASI ILIYOUWA LEO WILAYANI KAHAMA... SAMAHANI KWA PICHA

0 comments
Jamaa mmoja ambaye jina lake alikutambulika mara moja amechmwa moto asubuhi na kufariki papo hapo baada ya kujaribu kutaka kuiba vitu vikiwemo Laptop na vitu vyengine katika ajali iliyotokea leo asubuhi baada la Bus la Wibonela Express kupata ajali na kuua watu wanne .

Undani wa taarifa hizi utazipata baada ya muda mfupi.


BREAKING NEEEEWS..!! BASI LA WIBONELA LAPINDUKA WILAYANI KAHAMA ASUBUH HII NA KUUA.

0 comments



Huzuni na majonzi imetanda leo katika mji wa kahama baada ya basi la Wibonela Express linalofanya safari zake  Kahama -Dar kupinduka baada ya kutoka stand kuu ya kahama km chache toka stand katika eneo la Phantom  na kuua watu wanne.

Kwa taarifa za awali chanzo chz ajali hiyo ni mwendo kasi na Taarifa Rasmi na picha zaidi zitawajia hapo baadae.
 
  Endelea kufuatilia taarifa kupitia blog hii.
 













KIJANA ALIMEKUTWA AKIWA AMEKUFA KWENYE KORONGO LUBENGELA KIGOMA

0 comments

 
Katika hali ya kustajaabisha kijana mmoja alietambulika kwa jina moja la Yusuph (Me) mkazi wa Buzebazeba Ujiji amekutwa amekufa katika korongo la Lebengera jirani na Ofisi za CCM mkoa katika manispaa ya Kigoma Ujiji huku akiwa amejaa damu katika paji lake la uso
Mara baada ya Jeshi la Polis kufika eneo la tukio walimpekua marehemu na kumkuta na fedha taslimu kama elfu tatu hivi na karatasi ambayo haikujulikana maramoja imeandikwa nini
 tukio hilo limetokea jana Oktoba13 eneo tajwa hapo juu huku umati mkubwa ukiwa umefurika ili kumtambua na kushuhudia tukio hilo,

katika uchunguzi wa awali inasemekana tukio hilo limetokea jana usiku kwani kutwa nzima ya jana hapakuonekana mtu ambae amekufa
mmoja wa wananchi aliekuja kushuhudia tukio,na ambae ni mfanyakazi katika ofisi moja jirani na eneo la tukio( jina kapuni) amesema hii imekuwa ni mara ya pili kutokea tukio kama hili la mtu kukutwa ameuawa na kutupwa katika korongo hili,hivyo anaviomba vyombo vya usalama kuweka doria ya mara kwa mara eneo hili kwani eneo hili linakaribiana na Bar pamoja na Ofisi za Hazina Ndogo.

 Polisi wakichukua vielelezo katika picha


 
 Kutokana na eneo alilokutwa marehemu kuwa na miundombinu mibovu ya kumtoa walilazimika kutumia ngazi,hivyo waliomba msaaada wa ngazi kwa gari la 'emegency' la Tanesco na hapa ngazi ilikuwa inashushwa tayari mwili kupandishwa juu kupelekwa eneo husika.
polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo. 


 Mwili ukitolewa tayari kupelekwa kwenye gari la Polisi



 Mwili ukiingizwa kwenye gari la Polisi kuelekea 'Central Police' kwa taratibu zingine