Msafara wa magari ukitoka kuchukua mwili wa marehemu hospitali kuelekea nyumbani kwake.
Tajiri maarufu mjini Bukoba, Leonard Mtensa akichunguzwa na daktari.
KIFO cha
tajiri maarufu mjini Bukoba, Leonard Mtensa (50) ambacho kimetingisha
kanda nzima ya ziwa, kilichotokea dakika chache baada ya marehemu
kudaiwa kufanya mapenzi ndani ya gari lake, sasa mambo hadharani juu ya
kila kitu kilichotokea.
Tukio
hilo lililozua gumzo mjini Bukoba, lilitokea usiku Novemba 18, mwaka
huu ambapo imeelezwa kuwa marehemu ambaye ni baba wa familia, kabla ya
kupatwa na umauti, alikutwa ndani ya gari yake aina ya IST lenye namba
za usajili T. 982 CQG akifanya mapenzi na mchepuko wake aliyetajwa kwa
jina la Jackline Hassan (25) maeneo ya Buyekere mjini Bukoba.
Mwili wa marehemu, Leonard Mtensa ukitolewa hospitali ya mkoa wa Kagera kupelekwa nyumbani kwake kuzikwa jana.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa
mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio marehemu ambaye anamiliki Klabu
ya Linas, alidaiwa kunywa pombe kali aina ya Whisky Bond pasipo kula
vizuri huku akisumbuliwa na tatizo la presha hivyo wakati akifanya yake
ndani ya gari, ghafla presha ilipanda, akaanza kutapatapa.
“Si
unajua tena jamaa umri umeenda kidogo na anasumbuliwa na presha, sasa
inawezekana na kinywaji alichokunywa ndiyo kilitibua zaidi. Pombe ukiwa
hujala huku una tatizo la presha madhara yake ndiyo haya,” kilisema
chanzo chetu.
Mke wa marehemu akiwa haamini kama mumewe amefariki.
APEWA MSAADA
Baada
ya hali yake kubadilika ghafla, inadaiwa kuwa mpenzi wake badala ya
kukimbia kama ambavyo wengine hufanya, yeye alifanya juhudi kubwa
kujaribu kuokoa jahazi kwa kupiga simu kwa marafiki wa marehemu, lakini
kabla hawajafika, mtu mmoja alitokea na kumsaidia marehemu kumpeleka
katika kituo cha Afya cha CLCT-Ndolage.
AFIA NJIANI
Chanzo
hicho kilizidi kumwaga data kuwa, baada ya mtu huyo kujitolea
kumkimbiza hospitali, hali ya Mtensa ilizidi kuwa mbaya ambapo alifariki
kabla hajafika hospitali.
“Wakati
wanamchukua kwenye gari, mapigo ya moyo yalikuwa yakimwenda mbio sana
kabla hajafika hospitali akafariki,” kilisema chanzo chetu.
Binti aliyekuwa na marehemu.
HOFU KWA MREMBO
Chanzo
kilidai kuwa, baadhi ya marafiki wa marehemu waliingiwa hofu na mrembo
huyo na kuwa na wasiwasi wakihoji chinichini kwamba pengine alimpa
marehemu kitu kibaya.
“Marafiki
wa marehemu waliingiwa hofu sana na mazingira ya kifo, walikuwa
wakijiuliza isije kuwa mrembo aliyekuwa naye amempa kitu chenye
madhara,” kilisema chanzo chetu.
ASHIKILIWA NA POLISI
Kamanda
wa polisi mkoa wa Kagera, ACP Henry Mwaibambe alikiri kutokea kwa tukio
hilo ambapo alisema wanamshikilia Jackline kwa ajili ya upelelezi
zaidi.
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu.
AIBU, SIMANZI MSIBANI
Chanzo
hicho kilizidi kueleza kuwa, msibani nyumbani kwa marehemu maeneo ya
Kyakairabwa, kata ya Nyanga, waombolezaji walikuwa wakiona aibu
kuzungumzia kifo chake hadharani kwa kuona ni kashfa hasa kwa kuwa
marehemu alikuwa mtu anayeheshimika katika jamii.
Jeneza la marehemu, Leonard Mtensa.
“Unajua
hakuna mtu hata mmoja ambaye anataka kuongelea kifo cha baba huyo, hata
marafiki zake hawaongei kabisa kwani wanaona kuwa ni kashfa kwa sababu
Mtensa alikuwa ni mtu maarufu sana si kwa hapa Bukoba tu, bali hata
jijini Mwanza na kanda ya ziwa kwa jumla,” kilisema chanzo hicho.
WHISKY BOND IPOJE?
Ili
kutaka kufahamu uhusiano wa kilevi alichokutwa nacho marehemu na kifo
chake, waandishi wa habari hizo walimtafuta daktari mmoja mtaalamu wa
magonjwa ya binadamu, (jina linahifadhiwa) ambaye alisema kitendo cha
mwanaume kupoteza maisha akiwa anafanya mapenzi ni jambo la kawaida.
“Wako
watu wanaofariki wakiwa wanafanya tendo, inategemea, wengine wanakuwa
na historia ya magonjwa kama shinikizo la damu, sasa ile nguvu
inayotumika katika tendo na kama ugonjwa utatokeza wakati huo, uwezekano
wa kupoteza maisha ni mkubwa.
“Halafu
pombe kama hii ni kali, sasa kama mtu alikuwa na matatizo ya presha,
akawa amezidisha kiwango ni rahisi zaidi ku-collapse (hali kubadilika)
wakati wa tendo. Tatizo lingine linaweza kuwa ni aina ya vyakula
anavyokula kufuatia matumizi ya pombe yenye kilevi cha juu.
Mfano wa gari aina ya IST alipokutwa marehemu.
“Maana
unakuta mtu mwingine anakunywa kilevi kikali lakini hapendi kula, hili
nalo ni tatizo kubwa. Vinywaji vikali mara nyingi vinaendana na ulaji wa
vyakula vyenye mafuta kwa sababu hivi huenda kukausha damu,”
alisema.Marehemu aliyeacha mjane na watoto, alitarajiwa kuzikwa jana
mjini humo.
Chanzo Global