CCM WAIBUKA KIDEDEA KATIKA UCHAGUZI WA WENYEVITI NA MAKAMU WILAYA YA MBOGWE NA BUKOMBE




MKUU WA MKOA WA GEITA MAGALULA SAID MAGALULA  AKIWA NA VIONGOZI MBALIMBALI WA WILAYA YA BUKOMBE NA MBOGWE KATIKA KIKAO CHA KUVUNJA BARAZA LA MADIWANI NA KUCHAGUA MWENYEVITI NA MAKAMU WAO.



Viongozi wa halmashauri ya wilaya za mbogwe na bukombe mkoani geita wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano na kufuata kanuni za uongozi wa umma ili kuepuka migogoro katika halmashauri hiyo.

Hayo yamesemwa leo na mkuu wa mkoa wa geita magalula said magalula katika kikao cha kuvunja baraza la madiwani na kuchagua viongozi wapya kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya bukombe.
Magalula amesema viongozi watakaochanguliwa wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa na hivyo watumie vizuri nafasi zao ili kuleta maendeleo katika wilaya zao.

Katika kikao hicho ambacho kilikuwa cha kuvunja baraza la madiwani na kuchagua uongozi mpya mkurugenzi wa halmashauri ya bukombe lilian matinga amemtangaza mwenyekiti wa kuwa ni joseph kurya ccm aliyepata kura 12 kati ya kura 19.

Nafasi ya makamu mwenyekiti  imechukuliwa na lameck warangi kwa tiketi ya  ccm aliyepata kura 14 dhidi ya mpinzani wake yusuph fungameza aliyepata kura 5 kati ya kura 19.

Hata hivyo mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya mbogwe Sophia kumbuli amemtangaza mwenyekiti wa wa halmashauri hiyo vicent busiga na makamu wake nsika sizya waliopita bila vikwazo  kutokana na kutokuwa na wapinzani.

 MATUKIO KATIKA PICHA.

MKUU WA MOA WA GEITA AKIZUNGUMZA KATIKA KIKAO CHA KUVUNJA BARAZA LA MADIWANI BUKOMBE NA MBOGWE PEMBENI KULIA KWAKE NI MKURUGENZIWA BUKOMBE LILIAN MATINGA NA DC WA MBOGWE KUSHOTO KWAKE HUSNA MWILIMA.





0 comments: