Kampuni ya utafiti Resolute imekabidhi madawati 31 kwa shule ya msingi Kanegele.
| MENEJA WA KAMPUNI YA RESOLUTE WILLIAM HARMWORTH AKIJADILIANA JAMBO NA MKUU WA WILAYA MEJA MSTAAFU BAHATI MATALA KABLA YA KUKABIDHI MADAWATI SHULE YA MSINGI KANEGELE. |
| AKIKABIDHI MADAWATI KWA DIWANI WA KATA YA BUKANDWE LUTENI MSTAAFU HENLYMALISHI |
| MWALIMU MKUU AKIKABIDHIWA MADAWATI NA M/KITI WA |
| MWANDISHI NA MMILIKI WA BLOG HII HERIETH KATIKIROAKICHUKUA PICHA KWA AJILI YA BLOG |
| JONES NYAKWANA MJEOLOGIA KUTOKA RESOLUTE |
| HERIETH AKIWA NA WALIMU WA SHULE YA MSINGI KANEGELE |
RESOLUTE
WATUMIA MILIONI 47.7 KWA JAMII KATA YA BUKANDWE.
KAMPUNI
ya Resolute (Tanzania) Limited imetumia kiasi cha shilingi milioni 47.7 kwa
ajili ya kutoa huduma za kijamii katika kata ya Bukandwe;Wilaya ya Mbogwe
mkoani Geita.
Kiasi
hicho kilibainishwa na Meneja wa Kampuni hiyo;William Harmworth wakati
akikabidhi dawati 31 kati ya 45,katika shule ya msingi Kanegele iliyopo katika
kata ya Bukandwe ikiwa ni sehemu ya miradi minne iliyopanga kuitekeleza kwa
kipindi cha mwaka mmoja.
Harmworth
alisema mradi huo wa dawati umewagharimu kiasi cha shilingi Milioni 3.2 ambapo
wanataraji kuukamilisha kwa kukabidhi dawati zingine 14 ifikapo mwishoni mwa
mwezi huu.
“Tunathamini
swala la elimu ndio maana tumeweka kipaumbele ufadhili kukamilisha miradi
mbalimbali ya elimu na jamii ituunge mkono kwa faida ya nchi ya Tanzania”alisema
Harmworth.
Alisema
awali kampuni yake ilitekeleza mradi wa kisima cha pampu ya mkono kilichopo
maeneo ya shule ya msingi Kanegele kilichogharimu shilingi Milioni 28.2ambapo
mradi huo ulikamilika oktoba 30 mwaka jana.
Aliendelea
kusema miradi mingine ambayo imeshakamilika chini ya ufadhili wa kampuni yake
ni kuezeka na kukamilisha vyumba viwili vya madarasa na ofisi ya Mwalimu sambamba
na kukarabati chumba kimoja cha darasa ambapo vyote viligharimu kiasi cha
shilingi milioni 15.8.
Hata
hivyo Meneja huyo aliiomba jamii ya kata hiyo kuibua miradi ya maendeleo na
kuisimamia kwa uadilifu na kampuni yake haitosita kuwaunga mkono pindi watakapohitaji
msaada wao.
Nae
Diwani wa Kata ya Bukandwe;Luteni mstaafu Henly Malishi aliwakumbusha wenyeviti
wa vitongoji kuwahimiza wananchi wao
kuhakikisha wanatimiza kwa wakati ahadi yao ya kuchangia madawati ili kuwanusuru
vijana wao kutosoma wakiwa wamekaa chini.
Kampuni
ya Resolute (Tanzania)Limited inafanya utafiti wa madini ya dhahabu tangu mwaka
2003 katika kata ya Bukandwe,Nyakafuru na Nyakasaluma za Wialya Mbogwe mkoani
Geita.
0 comments: