HARAMBEE YA KATA YA BUSOKA YAFANAA.

Mh James Lembeli mbunge wa kahama akiongoz aharambee ya kuchangia nyumba ya mwalimu na shule ya sekondari ya Busoka iliyopo kata ya |Busoka wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga.


Usemi wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere wa “Ili maendeleo yawepo kunahitajika Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora”; leo umerejewa kwenye Kijiji Cha Kitwana Kata ya Busoka wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Tafakari hiyo imefanywa na mbunge wa Jimbo la Kahama James Lembeli, kufuatia malalamiko ya wananchi wa kijiji hicho kutelekezwa na uongozi wa kata hiyo katika shughuli za maendeleo na kubaki wakimtegemea Lembeli peke yake.
Katika mkutano huo wa Harambee ya ujenzi wa nyumba ya mwalimu wa shule ya sekondari, wananchi wamehoji kutokuwepo kwa Diwani Mabubu Mussa, huku afisa Mtendaji wa kata hiyo Antoni Kosta akiwa hana maandalizi yoyote.

Lembeli amelazimika kumpigia simu Mabubu akimwomba ataje mchango wake naye akataja shilingi 100,000=; huku Kosta akiaidi kutoa 80,000=, kiasi ambacho wananchi walikikataa huku viongozi hao wakisusia na kudai hawana uwezo wa kutoa zaidi ya hapo.

Katika Mkutano huo ambao Kwa mjibu wa Lembeli,  umevunja rekodi kwa wingi wa mahudhurio, wananchi wamesema hawana imani na uongozi wa kata ya Busoka na kwamba wangependa kujitegemea au kurudi kata ya zamani ya Malunga.

Lembeli amewaomba wananchi wa Kitwana bila kujali kama wametelekezwa, wajitolee kuchangia maendeleo yao na kwamba atakuwa nao bege kwa bega, kama alivyoanza kuchangia shilingi 2,000,000 za ujenzi wa msingi wa shule hiyo miaka mitatu iliyopita.

Amesema alichokiona yeye wananchi wako tayari, ardhi na siasa safi vipo, kinachokosekana kwao ni uongozi bora na kwamba imewapasa kuchagua kamati ya watu wanne wa kusimamia suala zima la ujenzi wa nyumba hiyo.

Wajumbe waliochaguliwa kwenye mkutano huo ni Andrea Juma, Shija Maganga, Lameki Bupamba na Christina Maganga wote wanatoka vijiji vya Sunge na Kitwana, huku Lembeli akimtaja Afisa Elimu ya Msingi- Taaluma Mwalimu Amani Sabasaba kuratibu ujenzi huo.

Katika harambee hiyo jumla ya Shilingi 6,072,050= zikiwemo shilingi 200,000 alizochangia Mwalimu Saba, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji shilingi 600,000=, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo 400,000= huku Lembeli akichangia shilingi 2,000,000= na mabati ya kuezekea.

Ziara ya Lembeli kwa awamu hii imehusisha zaidi ya vijiji 20 Jimboni mwake, na leo imehitimishwa katika kijiji cha Kitwana, tayari kwa kwenda kuhudhuria vikao vya Bunge mjini Dodoma, hadi hapo atakapotoa ratiba nyingine.

MATUKIO KATIKA PICHA 

MH LEMBELI AKIWA KATIKA MSONGAMANO MKUBWA WAKATI WAKIMLAKI LEO KATIKA HARAMBEE YA SHULE YA SEKONDARI YA KATA YA BUSOKA.

MH LEMBELI AKIWA NA WASWEZI WACHEZAJI WA NGOMA ZA ASILI


MKURUGENZI MSAIDIZI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA AKITOA MCHANGO WAKE NA M/KITI WA HALSHAURI.

HUYO MWENYE SHATI LA LIGHT-BLUE NDO MTENDAJI WA KATA AMBAYE WANANCHI WA KATA YAKE WAMEUKATAA MCHANGO WAKE PAMOJA NA DIWANI AMBAYE HAKUWEPO KATIKA HARAMBEE.


MH LEMBELI AKICHEZA NGONA NA WASWEZI.



 

0 comments: