AJALI YATOKEA KITULI,SHINYANGA
| GARI LILILOPATA AJALI ENEO AL KITULI |
Watu watano wamefariki dunia
na wengine wanne wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea leo katika eneo la kituli barabara ya tinde,isaka mkoani shinyanga.
Kamanda wa polisi mkoa wa
shinyanga evarist Mangala amekiri kutokea kwa ajali hiyo iliyohusisha toyota
hiace yenye namba za usajili T 920 CDM.
KAMANDA Mangala amewataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni peter mwigulu(27),ambaye ni mtendaji wa kijjii cha mwantini,Jackson Moses (21),Marco methew (21)Frijinia edward(23) na mwanaume anaekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 24-25 ambae jina lake halikufahamika.
amewataja majeruhi
katika ajali hiyo kuwa ni pamoja na john daud mkazi wa nyasubi kahama,stumai
shaban mkazi wa chato,Charles mpenda mkazi wa nyabukande na masumbuko matias
mkazi wa kakola.
Hata hivyo amesema chanzo
cha ajali hiyo ni mwendo kasi na kuwa dereva wa gari hilo amekimbia na
uchunguzi bado unaendelea.
Kamanda Evarist amewaonya
madereva wa magari ya abiria kuwa makini wawapo barabarani kwani ajali nyingi
zimekuwa zikitokea kutokana na kutokuwa makini barabarani na mwendo kasi.
| T920 CDM gari iliyopata ajali inavyonekana kwa nyuma. |
| Damu zikiwa zimejaa ndani ya gari hilo. |
0 comments: