ZITO NA WENZAKE WAPIGWA CHINI KATIKA UONGOZI

 

 

 

 

 

 

 

 

Zitto, Kitila na Samson Mwigamba wavuliwa vyeo vyote ndani ya chama

Kikao cha Kamati Kuu ndiyo kimeisha muda huu, na taarifa zilizopo ni kwamba kambi ya PM7 imevunjwa rasmi baada ya viongozi wake kuvuliwa vyeo vyote walivyo navyo ndani ya chama.

Waliovuliwa vyeo ni Zitto Kabwe, ambaye amevuliwa nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa chama pamoja na nafasi ya Naibu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Dr. Kitila Mkumbo yeye amevuliwa nafasi ya mjumbe wa kamati kuu.pamoja na Samson aliyekuwa Mwenyekiti huko Arusha

Kamati Kuu imewaandikia barua Zitto na Kitila, wajieleze ndani ya siku 14 kwanini wasifukuzwe uanachama.


0 comments: