EWURA yapandisha bei ya umeme, kuwagusa zaidi watumiaji wa majumbani...!!



EWURA yapandisha bei ya umeme, kuwagusa zaidi watumiaji wa majumbani

Mamlaka  ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza rasmi ongezeko la gharama za umeme, zitakazoanza kutumika rasmi January Mosi,2014. Ongezeko hilo limewagusa zaidi watumiaji wa majumbani wanaotumia chini ya unit 75 kwa mwezi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Slaam jana (December 23), Mkurugunzi Mdhibiti Uchumi wa EWURA, Felix Ngamlagosi alisema baada ya kupitia maombi yaliyopelekwa kwa mamlaka hiyo na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) October 1, mwaka huu, yaliyopendekeza ongezeko la bei kwa asilimia 67, mamlaka hiyo ilipitia sababu za Tanesco na maoni ya wadau na hivyo imeamua kupandisha bei ya nishati hiyo.
Amesema kuanzia mwezi ujao, wateja wadogo wa majumbani hasa vijijini ambao matumizi yao hayazidi unit 75 kwa mwezi, gharama zimeapanda kwa shilingi 40 kutoka shilingi 60 za sasa hadi shilingi 100 kwa unit moja.
Watumiaji wakubwa wa umeme majumbani, biashara ndogo ndogo, wenye mashine za kukoboa na kusaga nafaka, taa za barabarani, mabango, umeme umepanda kwa shilingi 85 kutoka shilingi 221 za sasa hadi 306 kwa unit moja, sawa na ongezeko la asilimia 40.

0 comments: