Hatimaye Barua ya Mwigamba yatua kwa msajili wa vyama vya Siasa Nchini...!!
Ofisi
ya Msajili wa vyama vya siasa nchini, imethibitisha kupokea barua ya
aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema )
mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.
Akizungumza
na paparazi wetu kwa njia ya simu, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji
Francis Mutungi, alithibitisha kupokea barua hiyo na kueleza kuwa ofisi
yake inaifanyiakazi.
“Tumepokea
barua ya Mwigamba, lakini siwezi kueleza kilichomo ndani yake kwa kuwa
ndiyo tunaifanyia kazi…tutawaita wanahabari kuwaeleza hatua
zilizochukuliwa na ofisi yangu,” alisema Jaji Mutungi.
| Msajili wa Vyama vya Siasa,Jaji Francis Mutungi |
Hivi
karibuni katika mkutano na waandishi wa habari, Mwigamba ambaye
amevuliwa madaraka yake yote ndani ya chama na wenzake, aliyekuwa Naibu
Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Kitila Mkumbo,
aliwasilisha malalamiko yake kwa msajili.
Katika
taarifa yake Mwigamba, amemuomba msajili kutoa mwongozo kuhusu
anachodai kuwa ni mgogoro wa kikatiba uliopo ndani ya Chama kufuatia
kipengele cha katiba kinachogusia ukomo wa uongozi kubadilishwa kinyume
na utaratibu.
“Katiba ya Chadema ya mwaka
2004 kipengele 5.3.2 (c) inasomeka ifuatavyo kuhusu Muda wa
Uongozi:Kiongozi aliyemaliza muda wa ungozi ana haki ya kugombea na
kuchaguliwa tena mradi awe anatimiza masharti ya kuchaguliwa kuwa
kiongozi kwa muda usiozidi vipindi viwili katika cheo kimoja kwa ngazi
moja,” alidai Mwigamba.
Hata hivyo,
alisema Katiba ya chama ya mwaka 2006 kipengele cha 6.3.2 ( c)
inayozungumzia muda wa uongozi unasoma: Kiongozi aliyemaliza muda wa
ungozi ana haki ya kugombea na kuchaguliwa tena mradi awe anatimiza
masharti ya kuchaguliwa kuwa kiongozi.
“Sentensi
kuhusu ukomo wa uongozi haipo. Ni kweli kuwa Marekebisho ya Katiba
yalifanyika mwaka 2006, lakini hoja ya kubadili kipengele hicho
haikuwepo na muhtasari zinaonyesha wazi kuwa kulikuwa hakuna mjadala wa
kipengele hicho au kuhusu suala zima la ukomo wa uongozi,” anadai.
Novemba
22, mwaka huu, Kamati Kuu iliwavua madaraka viongozi hao na kuwataka
wajieleze kwa maandishi ndani ya siku 14 baada ya kudaiwa kuhujumu chama
kwa kuandika waraka wa siri unaodaiwa pamoja na mambo mengine,
kuwadhalilisha viongozi wakuu wa Chadema.
0 comments: