Akizungumza kwa uchungu, baba wa mtoto huyo, Joseph Isaac alisema mwanaye alibakwa na mfanyakazi huyo wa nguruwe aliyemtaja kwa jina la Fabiano baada ya kumuahidi kuwa atampa pipi.
“Siku hiyo nilirudi nyumbani nikamkuta mwanangu anachemka homa kali, nikamwambia mama yake amuogeshe tumpeleke hospitali kwani tulikuwa tumeshampatia dawa ya kutuliza lakini haikumsaidia,” alisema baba huyo.
Mama wa mtoto huyo aliyetajwa kwa jina la Elizabeth, alimuogesha mwanaye na kugundua kuwa alikuwa amevimba sehemu za siri kutokana na majeraha aliyopata na alipombana ndipo alipomtaja mfanyakazi huyo wa nguruwe.
kwa mjumbe wa eneo hilo, Anna Kosmas ambaye alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuambatana na waandishi hadi nyumbani kwa mtuhumiwa ambapo walielezwa kuwa ametoweka.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Marietha Minangi aliahidi kufuatilia suala hilo kwani limesharipotiwa kituoni hapo na atahakikisha mtuhumiwa anakamatwa.
Wakati huo huo, mtoto mwingine mkazi wa Makabe, Dar aliyejulikana kwa jina la Sara (10) amesimulia jinsi alivyokuwa akibakwa mara kwa mara na mlinzi wa baa anayejulikana kwa jina la Athuman.
Akizungumza kwa masikitiko, mtoto huyo alisema kila siku huwa anaenda kuangalia video kwenye Pub ya Jack anayolinda mlinzi huyo ambapo wakati wa kurudi inakuwa ni usiku ndipo mlinzi huyo anapotumia muda huo kumaliza haja zake.
Alisema mlinzi huyo alikuwa akimkamata kwa nguvu na kumfunga kamba mkononi, miguuni na kumziba mdomo huku akimtishia kuwa akipiga kelele, atamchoma mkuki kitendo ambacho kilimsababisha mtoto aogope kumwambia hata mama yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments: