Wakulima waikataa mbegu ya Pamba aina ya Qtoni kuwa haina manufaa kwao.
| Wakuliwa wa Pamba wakiwa katika kikao na wadau wao juu ya kutafuta mbinu za kumaliza changamoto zinazowakabili wakulima wa Pamba katika Wilaya ya Kahama |
Wakulima wa zao la pamba
wilayani kahama mkoani Shinyanga wameilalamikia serikali kutokana na kuruhusu matumizi
ya mbegu za aina ya Qutoni ambayo imekuwa ikiwasumbua wakati wa kuota.
Malalamiko hayo yametolewa LEO
na wakulima wawakilishi kutoka katika kata mbalimbali katika kikao cha siku
moja cha wadau wa pamba kilichofanyika katika ukumbi wa cartas kahama mjini.
Wakieleza changamoto kubwa
inayowakabili kuwa ni mbegu mpya ya Quton isiyokuwa na manyoya ambayo haioti na
hivyo kuwafanya wakulima kupoteza muda na fedha lakini pia kuwafanya wakulima
kukata tamaa ya kuendelea kulima zao hilo.
Mwakilishi wa wakulima Joseph Mayunga
kutoka kata ya Nyandekwa amesema kuwa walitumia mbegu hiyo mpya kutokana na
maelezo kuwa inatoa kilo 1400 badala ya kilo 800 iliyokuwa ikipatikana kwa mbegu
ya zamani matokeo yake mbegu haikuota kabisa.
Ameendelea kusema kuwa hali
hiyo ndio inayokatisha tama wakulima kuendelea kulima pamba kwa
wingi.iliyomkatisha tmWakulima hao -
Upande wake Jimmy Luhende mdau
kutoka Shirika lisilo la kiserikali ADLG lililopo jijini Mwanza amewataka
wakulima hao kutambua changamoto zinazowakabili katika zao la Pamba na kisha
kukaa na serikali katika kuzitafutia suruhu.
Luhende amesema leongo la
kukutana na wakulima ni kutafuta mbinu za kumaliza changamoto zinazowakabili wakulima
wa Pamba.
HABARI KATIKA PICHA.
| Wakulima wa pamba wakiwa katika kikao ukumbi wa cartas kahama. |
| Mwenyekiti wa chama cha MVIWATA Elizabeth Masanja na Mwalimu ambaye pia ni mkulima wa zao la Pamba. |
| Mwezeshaji wa kikao hicho kutoka ADLG-Achions for Democracy and Local governs Mr Luhende Jimmy kutoka Mwanza akiongea na wakulima . |
| Bwana Mayunga Masele mkulima wa Pamba tanggu mwaka 1983 asiyejua aina ya mbegu anazozitumia kipindi chote alipokuwa akilima zao hilo. |
| Mkulima Bora wa Pamba kutoka Saba sabini aliyewahi kuzawadiwa TRekta na Mh Rais wa Jamuhuri a Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akitoa chanamoto zinazowakabili katika ilimo cha pamba. |
| katibu wa chama cha wakulima wa Pamba wilayani kahama TACOGA bwana Paul Ntelya akisikiliza kwa umakini . |
0 comments: