MWANAMKE NAYE AUWAWA NA WANANCHI KWA KUIBA MAHINDI MKOANI GEITA...!!
Mtu mmoja Mwanamke aitwaye
Savina Sambila anayekadiriwa kuwa na miaka 20-22 mkazi wa Kitongoji cha Ilolangulo
Wilayani Geita, mkoani
Geita, amepigwa hadi kufa na hatimaye kuchomwa moto na wananchi kwa tuhuma za
wizi wa mahindi.
| Mwili wa Savina Sambila akiwa amekokewa moto na wananchi wenye hasira kali baada ya kumuua |
Tukio hilo limetokea
majira saa nane usiku wa kuamkia leo baada ya Sambila kukutwa akiiba Mahindi
katika shamba la Milika
Migeka lililopo pembeni ya nyumba yake kijini humo.
| Mwenyekiti wa kitongoji cha Ilolangulo Bw. Abel kideshe (kulia) na makamu wake Deus Lutubija wakitoa magogo kwenye mwili wa marehemu. |
Imeelezwa kuwa baada ya
kumkamata Sambila walimtaka kupiga yowe na aliposhindwa ndipo walipoanza kumpiga hadi
kupoteza maisha papohapo, na kisha kumchoma moto kabla ya viongozi wa kitongoji
hicho kufika na kuuzima.
Mwenyekiti wa kitongoji hicho
Abeli Kideshe amewataka
wananchi kutokujichukulia sheria mkoni pindi panapotokea matukio kama hayo, bali
wawapeleke watuhumiwa kwenye vyombo vya sheria ili haki iweze kutendeka.
| Kiroba cha mahindi aliyokuwa ameiba marehemu Sabina Sambila |
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Geita
Kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Leonard Paul amethibitisa kutokea kwa
tukio hilo na kueleza kuwa uchunguzi unaendelea ili kuwabaini waliohusika na
kitendo hicho ili sheria ichukue mkondo wake.
Tukio hilo limekuja siku chache tu
baada ya watu watano kuwawa na kuchomwa moto katika kitogoji cha Nyantorotoro A
wilayani humo baada ya kuiba rambirambi kiasi cha shilingi 65,000.
Taarifa na Valence Robert - Geita
0 comments: